Mtoto wa Michael Jordan, akamatwa Florida baada ya kukutwa na dawa za kulevya

Mtoto wa Michael Jordan, akamatwa Florida baada ya kukutwa na dawa za kulevya

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Marcus Jordan, mtoto wa mwanamichezo maarufu wa mpira wa kikapu, Michael Jordan, amekamatwa Florida kwa tuhuma za kuendesha gari akiwa amelewa na kumiliki dawa za kulevya aina ya cocaine. Polisi walimkamata baada ya kugundua gari lake, Lamborghini, limekwama kwenye reli za treni, ambapo uchunguzi wa awali ulionesha dalili za ulevi na uwepo wa dawa hizo haramu.

Soma, Pia: Mtoto wa Michael Jordan, amepigwa picha akiwa anatumia dawa za kulevywa aina ya Cocaine

Kwa mujibu wa taarifa za polisi, Marcus alikataa kushirikiana na maafisa wa usalama wakati wa ukamataji, hali iliyosababisha kuzuiliwa kwake. Baada ya upekuzi wa gari lake, dawa hizo za kulevya zilipatikana, na kwa sasa anashikiliwa akisubiri kufikishwa mahakamani.

Hii si mara ya kwanza Marcus kukumbwa na matatizo ya kisheria. Mwaka 2012, alikamatwa kwa utovu wa nidhamu na kupinga kukamatwa akiwa amelewa. Pia, mwaka jana alihusishwa na video iliyodaiwa kumuonesha akitumia dawa haramu wakati wa mapumziko yake Ufaransa, jambo lililozua mjadala kwa mashabiki wa familia ya Jordan.

Hadi sasa, familia ya Jordan haijatoa tamko rasmi kuhusu tukio hilo, huku wengi wakisubiri hatua za kisheria zitakazochukuliwa dhidi yake.

 
Watoto wa watu mashuhuri huwa wanaishia pabaya sana. Malezi yao, ukuwaji wao, socialisations zao daima hutegemea jinsi wazazi walivyo na circles zao, sasa wanapokuja kuwa exposed into new environments akili zao na majibu yao huwa ya vilevile kama wako kwenye circles za wazazi wao. Tatizo huzaliwa.......
 
Watoto wa watu maarufu baadhi ni changamoto kweli mfano jack chan mtoto wake kamshindwa ni shida kwakweli!?
 
Back
Top Bottom