Mtoto wa miezi 3.5 hanyonyi

Mtoto wa miezi 3.5 hanyonyi

nusuhela

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2014
Posts
5,915
Reaction score
7,210
Habari za hapa jf?
Samahani naomba kujua kama ni tatizo au ni kawaida kwa mtoto wa umri wa miezi 3.5 kunyonya kwa kubeep. Yaani ananyonya kidogo sana alafu anakua hataki tena.

Bado hajaanza kula chochote zaidi ya kunyonya maziwa ya mama yake. Hii hali ni wiki ya pili sasa.

Wiki moja iliyopita akiakua na tabia hiyo, baada ya siku tatu akawa ananyonya kama kawaida. Leo hii ameanza tena
 
May be mama alitumia madawa makali yakapelekea maziwa kuwa na harufu

Au hashibi basi anaona bora asinyonye
 
Poleo ndugu jaribu kuwaona wataalamu wa afya, pia washirikishe kina mama watu wazima au ndugu zako wenye uzoefu na malezi
 
Pengine Ana homa. Ni vema kumuona daktari na kwa umri Huo usikimbilie jf kuomba msaada muone daktari wa watoto.
Umri Huo bado Sana kuweza kujichukulia Hatua ya kumtibu kwa uzoefu. Nenda kituo cha afya.
Hope atakuja kuwa Sawa.
 
Kawaida tu atakuwa mama hana maziwa ya kutosha au alimmistreet muda fulani akamind.. au kama ni mfanyakazi ya wezekana anachopewa anashiba na anaona Uvivu kuvuta nyonyo ya mama mkuu kawaida tu
 
Back
Top Bottom