Uwoga wako tuu. Mtoto wa miezi minne bado ni mdogo sana naweza kulia hata akiwa amebebwa na mama yake. Ukiwa na muda jitahidi akuone wakati akiwa na mama yake ata kuzoea na utasahau yote. Ila ukianza tu kumkaribisha shetani kichwani mwako uka anza kumkagua kwa macho ya ukali na roho ya husuda anaweza kulia mpaka azimieHabari!
Nina mtoto wa kiume ana miezi minne sasa. Tatizo ni kwamba huwa analia sana nikimshika/nikimbeba, lakini akishikwa au kubebwa na mama yake ananyamaza na mwisho wa siku anakua kawaida tu. Kuna aliyewahi kupitia hili, suluhu ilikua nini? Au sababu ya hili ni nini, maana linaninyima raha sana hata siwez kufurah na mtoto wangu.