Kama mbunge kweli anatetea wanyonge,na ameona ni vyema kumpeleka mtoto wake shule yenye mkondo wa kiingereza(English medium school),basi ni vyema akapeleka muswada binafsi bungeni "Serikali ibadilishe mfumo wa elimu ili Watanzania waweze kunufaika na shule kuwa na michepuo ya kiingereza",na aombe kujua ni lini Serikali itafanya utafiti na tathimini ya namna ya kubadili mfumo wetu ili nchi iwe na vijana wenye kuweza kushindana kimataifa katika kutafuta maisha na fursa katika nchi za mataifa mengine.