Mkuu wa zamani wa Jeshi la Ardhini la Uganda Muhoozi Kainerugaba ambaye pia ni Mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, leo October 19,2022 amerejea tena kauli yake ya kuwahamiza Vijana wa Afrika Mashariki kuunga mkono hoja yake ya kutaka Nchi za Afrika Mashariki ziungane na kuwa Taifa moja.
“Vijana wenzangu wa Afrika, nikiwa kama Kiongozi wenu ambaye mmenichagua wenyewe, nawahimiza kuuona umuhimu wa kushinikiza kwa haraka muungano wa Nchi za Afrika Mashariki, huu ni mpango wetu mdogo wa kisiasa, mipango mingine nitawapa mwongozo”
Itakumbukwa October 04,2022 Muhoozi alisema ameongea na Baba yake Rais Museveni kuhusu mpango wa kuifanya Afrika Mashariki kuungana na akasema mipaka iliyopo iliwekwa na Wakoloni na hakuna haja ya kuendelea kuiacha badala yake Nchi za Afrika Mashariki zinapaswa kuifuta mipaka hiyo na kutengeneza Taifa moja huku akisema Afrika Mashariki ikiwa Taifa moja anapendekeza Baba yake Museveni ndiye awe Rais wa Muungano huo.
Kauli ya Muhoozi inakuja siku mbili tu tangu Baba yake Rais Museveni aseme amemzuia Mtoto wake kuzungumzia Mataifa mengine au kuongelea siasa kupitia akaunti yake ya Twitter lakini jana Muhoozi alijibu kwamba yeye ni Mkubwa (sio Mtoto) na hakuna yoyote anayeweza kumpangia cha kufanya.
Credit: Millard Ayo UPDATES