Mtoto wa Rais Museven afikishwa mahakamani kwa kuutaka Urais wa Uganda

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
1652182813255.png

Picha: Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba

Mtoto wa Rais Museven afikishwa mahakamani kwa kuutaka Urais wa Uganda

Mahakama ya kikatiba ya Uganda imemtaka mtoto wa Rais Yoweri Museveni, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba, kujibu shtaka analotuhumiwa la kueleza nia yake ya kuwania urais akiwa bado anahudumu katika jeshi la nchi hiyo, tovuti ya Daily Monitor imeripoti.

Wakili wa haki za binadamu Gawaya Tegulle aliiomba mahakama katika mji mkuu, Kampala, kumzuia Jenerali Kainerugaba kufanya shughuli za kisiasa akiwa bado anatumikia jeshi.

Gawaya pia anataka jenerali huyo afunguliwe mashtaka ya uhaini kufuatia madai yake ya njama ya kumrithi babake kwa kutumia mbinu "haramu".

Jenerali Kainerugaba, kamanda wa jeshi la nchi kavu la Uganda, ana siku 10 kuwasilisha majibu yake. Mnamo tarehe 2 Mei, alitangaza mipango ya kuzindua mpango wa kisiasa, na kuchochea uvumi kwamba alinuia kumrithi babake wa muda mrefu.

Mnamo Machi 8, alitangaza kustaafu kutoka kwa jeshi kwenye Twitter lakini Rais Museveni alikataa. Rais Museveni amekanusha kumuandaa mwanawe kuchukua wadhifa wake.

Chanzo: Global Publishers
 
Hapo hamna kesi ni wana mfanyia kampeni kimchongo. Rais kumfunga mwanae aliyemuandaa na kumpeleka ktk mafunzo huku na huko pamoja na kumpa cheo cha juu ktk usalama wa nchi.

Haikuwa bahati mbaya, kujiuzulu mtandaoni tena baada ya kutoka katika ziara ya kidiplomasia nchini Rwanda.

Hizi kwangu ni propaganda zenye kumfanyia kampeni/kumtangaza kwa waganda.
 
Kumbe huko Uganda mtu kueleza nia ya kugombea Urais ni kosa??!!
 
Huyu jamaa kila baada ya muda ana tweet kuhusu kuutaka uraisi.

Last month alifanya birthday Kagame akahudhuria.

Anamuhusudu sana Kagame.

Ila jamaa naona bado ana akili za utoto mwingi ukifuatilia post zake.
 
Bado kitambo kidogo na hapa bongo tutasikia mtoto wa rais mstaafu anatangaza nia ya kugombea urais 😀
 
View attachment 2219011
Picha: Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba

Mtoto wa Rais Museven afikishwa mahakamani kwa kuutaka Urais wa Uganda

Mahakama ya kikatiba ya Uganda imemtaka mtoto wa Rais Yoweri Museveni, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba, kujibu shtaka analotuhumiwa la kueleza nia yake ya kuwania urais akiwa bado anahudumu katika jeshi la nchi hiyo, tovuti ya Daily Monitor imeripoti.

Wakili wa haki za binadamu Gawaya Tegulle aliiomba mahakama katika mji mkuu, Kampala, kumzuia Jenerali Kainerugaba kufanya shughuli za kisiasa akiwa bado anatumikia jeshi.

Gawaya pia anataka jenerali huyo afunguliwe mashtaka ya uhaini kufuatia madai yake ya njama ya kumrithi babake kwa kutumia mbinu "haramu".

Jenerali Kainerugaba, kamanda wa jeshi la nchi kavu la Uganda, ana siku 10 kuwasilisha majibu yake. Mnamo tarehe 2 Mei, alitangaza mipango ya kuzindua mpango wa kisiasa, na kuchochea uvumi kwamba alinuia kumrithi babake wa muda mrefu.

Mnamo Machi 8, alitangaza kustaafu kutoka kwa jeshi kwenye Twitter lakini Rais Museveni alikataa. Rais Museveni amekanusha kumuandaa mwanawe kuchukua wadhifa wake.

Chanzo: Global Publishers
Ninakumbuka kisa cha Oedipus
 
Kumbuka ni mjeshi huyo.

Kwani mjeshi hana utashi wa kibinadamu??!--- yaani mtu akishakuwa mjeshi basi anakuwa kama Robot na hivyo hastahili mahitaji na utashi wa kibinadamu??!---- is it conceivable!!
 
Mkuu, Katiba yao ndiyo inaelekeza hivyo. Kama anautaka U'NYERERE wa huko kwao, basi awe nje ya jeshi!
 
Si ndio nasema ni sheria ya kipuuzi hiyo, ni sawa na kumkataza mwanaume rijali asioe. Hiyo ni sheria inayopingana na demokrasi ya mtu kuchaguliwa kuwa kiongozi.
 
Huyu jamaa kila baada ya muda ana tweet kuhusu kuutaka uraisi.

Last month alifanya birthday Kagame akahudhuria.

Anamuhusudu sana Kagame.

Ila jamaa naona bado ana akili za utoto mwingi ukifuatilia post zake.
Kweli kabisa mkuu,mm pia huwa namfuatilia Sana,yaani hajakomaa,ana utoto mwingi.
 
Si ndio nasema ni sheria ya kipuuzi hiyo, ni sawa na kumkataza mwanaume rijali asioe. Hiyo ni sheria inayopingana na demokrasi ya mtu kuchaguliwa kuwa kiongozi.
Nafikiri kwa kuzingatia cheo chake jeshini inamaanisha ana influence kwa walio chini yake pia hivyo anavyosema nia yake huku bado yupo ndani ya jeshi yawezekana anataka kufanya mapinduzi
 
Back
Top Bottom