Kama hakuna kiongozi wa jeshi aliyewahitangaza nia ya kuwania urais ndio tuseme kutangaza nia ukiwa katika hayo madaraka ni kosa???!!
Huyo aliyetamani u-IGP huyo alifanya kosa kwani cheo cha U IGP hakigombewi kama cheo cha Urais hivyo huyo ilitakiwa asipewe hicho cheo tu na hiyo ingetosha kuwa ndio adhabu yake na si vinginevyo.
Cheo cha uraisi mtu anapigiwa kura, yaani ni watu ndio wanaokuchagua kwa kukuona unafaa sasa mtu anapotangaza nia ni sawa na kuwaambia wapiga kura kwamba na yeye anataka kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho na hivyo anaweza kuona/prediction ya upepo jinsi jamii inamuonaje.
Sio kosa kwa mtu yeyote kutangaza nia ya kugombea cheo kinachotolewa na radhaa ya umma, kama ipo sheria inayowadhulumu watu wa kada fulani kutangaza nia hiyo ni sheria ya kidhalimu dhidi ya haki ya kila mtu, haki ya kuchagua na kuchaguliwa.
Hebu niambie hivi huyo mwanajeshi hana haki ya kuchagua kiongozi katika uchaguzi mkuu??!!, kama anayo haki vipi akose haki ya kutangaza nia ili hapo baadaye umma umchague au usimchague kipitia njia.ya demokrasia??!!.
Hili jambo watu mnalitazama negative sana kuliko positive kiasi kwamba mnataka kuwanyima watu fulani haki yao ya kidemokrasia kisa tu watu hao wanawadhifa fulani--- wadhifa umegeuka laaana na mwiko!!!