Mtoto wa Rais Paul Biya amewaomba wananchi wa Cameroon wasimchague tena baba yake kuwa rais

Mtoto wa Rais Paul Biya amewaomba wananchi wa Cameroon wasimchague tena baba yake kuwa rais

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
G1NP6KVWAAEN8f9.png


Brenda Biya, binti wa Rais wa Cameroon Paul Biya, amewaomba wananchi wa nchi hiyo kutompigia kura baba yake katika uchaguzi wa Oktoba 2025.

Kupitia moja ya matangazo ya moja kwa moja kwenye TikTok, akitumia jina la utani “King Nasty,” alimkosoa kwa uongozi wake wa miaka 43 akisema umesababisha umasikini, ukosefu wa ajira na kudorora kwa maendeleo.

Hatua hii isiyo ya kawaida ni mara ya kwanza katika historia ya siasa za Afrika mtoto wa rais aliyepo madarakani kuupinga waziwazi utawala wa mzazi wake na kuwasihi wapiga kura wasimchague. Paul Biya, mwenye umri wa miaka 92, ambaye ni miongoni mwa viongozi waliotawala muda mrefu zaidi duniani, anakabiliwa na tuhuma za kiimla, ufisadi na chaguzi zenye utata.

Wakosoaji wanasema Brenda, anayefurahia maisha ya kifahari ughaibuni na akiwa na uhusiano mgumu kifamilia, huenda mawazo yake hayaonyeshi kikamilifu changamoto halisi zinazowakabili raia wa kawaida wa Cameroon.

Chanzo: African Hub
 
Hahaaaa. Ile ni style ya uchoraji wa wakati ule. Zamani nilikuwa natatizika sana nikizioni. Mimecheka sana🤣
Kiongozi, zile picha nikiziangalia huwa sizielewi kabisa. Huwa najiuliza, inamaana Sir Isaac Newton, Jethro Tull, King Louis na Marie-Antoinnete walikuwa na sura kama za wenye utindio wa akili (autism)? Kumbuka hawa wenye utindio wa akili wa visura fulani hivi vya kufanana awe Tanzania,Burundi au Uturuki. 😂🤣
 
Back
Top Bottom