Mgombea Ubunge Jimbo la Makunduchi, Wanu Hafidh Ameir amesema Wananchi wa Kizimkazi wameomba Mashine maaalum za kuchimba Makaburi kutokana na ardhi yao kuwa ngumu ya Mawe hali inayowapa tabu wakati wa kuchimba hivyo kwa kushirikiana na Viongozi wenzake watakwenda kununua Mashine tatu ili kuondoa changomoto.
Ameyasema hayo huko Kiwanja vya Pwani Kizimkazi Mkunguni ukiwa sehemu ya mwendelezo wa Mikutano ya Kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, ambapo amesema Wana Makunduchi wanapaswa kuwachagua ili kuwaletea maendeleo na kuwaondolea changomoto zote zinawakabili kwani wamedhamiria kuwatumikia Jimbo la Makunduchi.