Mtoto wa Simbachawene alimwa faini ya tsh. 250,000/=

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,775
Reaction score
29,746
images (1).jpeg

Mfanyabiashara, James Simbachawene (24) ambaye ni mtoto wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene, amehukumiwa kulipa faini ya sh. 250,000 na kufungiwa leseni yake ya udereva kwa miezi sita baada ya kukiri makosa matatu.

Mtoto huyo amefikishwa mahakamani hapo leo Jumatano Agosti 24, 2022 jioni na kusomewa mashtaka yake na wakili wa serikali, Daisy Makakala, mbele ya Hakimu Mkazi Aron Lyamuya.

Mashitaka hayo ni pamoja na kuendesha gari kwa hatari, kuendesha gari akiwa amelewa na kuendesha gari bila kuwa na bima.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Simbachawene alikiri na ndipo hakimu Lyamuya alipoahirisha kesi ili kumwandikia hukumu.

Baada ya muda mfupi, ndipo hakimu Lyamuya alimhukumu Simbachawene kulipa faini ya Sh100,000 kwa kosa la kuendesha gari kwa hatari, Sh100,000 kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa na Sh50,000 kwa kosa la kuendesha gari bila kuwa na bima.

Pamoja na faini hiyo, leseni ya Simbachawene imefungiwa kwa miezi sita.

Chanzo: Mwananchi News Paper
 
Kwa mujibu wa sheria.

Sasa ngoja wajhomba waamke na stress zao wakwambie adhabu ndogo.
Kwa mjibu wa sheria kwa Simbachawene, sio wewe BUFA.

WEWE jichanganye road ufanye huo ujinga kisha ukawatukane mapolisi kuwa ni wasenge, ndio utapata jibu la kuwa hiyo kwa mujibu wa sheria (250K) haikuhusu.

NB; KWANZA picha linaanza unasota mahabusu mwaka mzima, wakati mwenzako hajakaa hata week😄.
 
Mimi ningemaliza mchezo pale plae. Hii ishu imekuzwa sababu dogo ni mtoto wa waziri ila hivi visa kila siku vinatokea road, traffic wanapozwa then wote mnasonga mbele kama injili
 
Utapewa kesi ya Kutukana matusi, utapewa kesi ya kumzuia askari kufanya majukumu yake, na jinai zingine kadhaa tu hivi. Hiyo miezi anayofungiwa kuendesha gari lakin anakua uraiani, kama ndio wewe utakua uko mahabusu ukiwa ushakula virungu vya kutosha tu.
 
Baada ya muda mfupi, ndipo hakimu Lyamuya alimhukumu Simbachawene kulipa faini ya Sh100,000 kwa kosa la kuendesha gari kwa hatari, Sh100,000 kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa na Sh50,000 kwa kosa la kuendesha gari bila kuwa na bima.

Pamoja na faini hiyo, leseni ya Simbachawene imefungiwa kwa miezi sita.
Credit; Mwananchi News Paper
Alilipa fine? Receipt iko wapi tunaomba tuione maana nchi yetu kwa sarakasi haijambo.
 
Mimi ningemaliza mchezo pale plae. Hii ishu imekuzwa sababu dogo ni mtoto wa waziri ila hivi visa kila siku vinatokea road, traffic wanapozwa then wote mnasonga mbele kama injili
Una uhakika wa kufikishwa mahakamani ndani ya siku mbili kama huyo mtoto ili ukailipe hiyo 250K, IKITOKEA UMELAZIMIKA KUSHIKILIWA NA POLICE?

ASSUME hizo mbinu zako za kuwapoza maafisa zimedunda, unadhani muda huu kesi yako ingekuwa imesikilizwa?

Nataka uione tofauti yako BUFA na mtoto wa Chawene.
 
Back
Top Bottom