Mtoto wa Simbachawene alimwa faini ya tsh. 250,000/=

Mtoto wa Simbachawene alimwa faini ya tsh. 250,000/=

Jambo la msingi linabaki palepale kuwa hiyo Jeuri aliipata wapi?

Viongozi mnao teuliwa kumbukeni kuwa vyeo mlivyo pewa ni dhamana tu, acheni kuwalea watoto wenu vibaya kwa kuwajengea dhana mbaya kuwa wewe ndio kila kitu.

Tulitegemea adhabu iwe kifungo jela badala ya kulipa faini ili iwe fundisho kwa wale wote wanao jiona kuwa wao wapo juu ya sheria.
 
Teh teh teh teh... Tanzania bwana nchi ya kijinga kabisa.

Sijasema mtoto wa Simba ana makosa ila mifumo yetu ni mibovu kabisa. Policcm
Traffic case ni kesi za kawaida sana hata angegonga akaua watu 10 bado adhabu yake ingekua siyo kubwa kesi za barabarani hazina mambo mengi labda uwe hauna lesen ndo inakuaga ngumu kidogo hata makosa aliyo yafanya huyo jamaa ni makosa ya kawaida tu ila kwakua ni mtoto wa kiongozi ndo maana imechukuliwa tofauti ila Sheria ni 1 tu
 
Mfumo gani wa kijinga? Traffic case ni kesi za kawaida sana hata angegonga akaua watu 10 bado adhabu yake ingekua siyo kubwa kesi za barabarani hazina labda uwe hauna lesen ndo inakuaga ngumu kidogo hata makosa aliyo yafanya huyo jamaa ni makosa ya kawaida tu ila kwakua ni mtoto wa kiongozi ndo maana imechukuliwa tofauti ila Sheria ni 1 tu
Kwa hiyo yale matusi aliokua akitukana ni traffic case nayo?
 
Jambo la msingi linabaki palepale kuwa hiyo Jeuri aliipata wapi?

Viongozi mnao teuliwa kumbukeni kuwa vyeo mlivyo pewa ni dhamana tu, acheni kuwalea watoto wenu vibaya kwa kuwajengea dhana mbaya kuwa wewe ndio kila kitu.

Tulitegemea adhabu iwe kifungo jela badala ya kulipa faini ili iwe fundisho kwa wale wote wanao jiona kuwa wao wapo juu ya sheria.
Tatizo Afrika sio kama ulaya Afrika matajiri hawafungui
 
ningekuwa mimi pamoja na yote hayo, ningejiuzulu nafasi yangu niliyo teuliwa ili kuonyesha uwajibikaji kwa kitendo alicho fanya mtoto wangu haswa pale alipo tumia cheo cha Baba yake kujigamba kuwa yupo juu ya sheria na anaweza fanya makosa bila kuchukuliwa hatua kwa kutegemea wadhifa wa Baba yake.

viongozi wetu kuweni na utamaduni wa kuwajibika nyinyi wenyewe kwa makosa mbalimbali yanayo jitokeza, sio mpaka unyofolewe.
 
Traffic case huwa nyepesi sana

Ukijiandaa unaimaliza....kwenda jela ni uzembe wako tu

Ova
 
Kikubwa kanuni, taratibu na Sheria zimefuatwa tofauti na hapo Hakimu ndo aulizwe, Tanzania ngumu sana mpaka hukumu yabishiwa
 
Kwa hiyo yale matusi aliokua akitukana ni traffic case nayo?
Kama alietukanwa hajafungua kesi hawezi kuhukumiwa kwa kesi ambayo hajapelekwa nayo ilibidi alie tukanwa akafungue kesi ya jinai Kutoa lugha ya matusi lakin pia bado ni kesi ndogo tu inamalizwa hapo mahakama ya mwanzo
 
Back
Top Bottom