Mtoto wa Simbachawene alimwa faini ya tsh. 250,000/=

Mtoto wa Simbachawene alimwa faini ya tsh. 250,000/=

View attachment 2333685
Mfanyabiashara, James Simbachawene (24) ambaye ni mtoto wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene, amehukumiwa kulipa faini ya Sh250, 000 na kufungiwa leseni yake ya udereva kwa miezi sita baada ya kukiri makossa matatu.

Mtoto huyo amefikishwa mahakamani hapo leo Jumatano Agosti 24, 2022 jioni na kusomewa mashtaka yake na wakili wa Serikali, Daisy Makakala, mbele ya Hakimu Mkazi Aron Lyamuya.

Mashitaka hayo ni pamoja na kuendesha gari kwa hatari, kuendesha gari akiwa amelewa na kuendesha gari bila kuwa na bima.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Simbachawene alikiri na ndipo hakimu Lyamuya alipoahirisha kesi ili kumwandikia hukumu.

Baada ya muda mfupi, ndipo hakimu Lyamuya alimhukumu Simbachawene kulipa faini ya Sh100,000 kwa kosa la kuendesha gari kwa hatari, Sh100,000 kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa na Sh50,000 kwa kosa la kuendesha gari bila kuwa na bima.

Pamoja na faini hiyo, leseni ya Simbachawene imefungiwa kwa miezi sita.
Credit; Mwananchi News Paper
Lile kosa la kutukana tusi maarufu naona limesahauliwa.. Na hata lile la kukataa kutii sheria bila shuruti pia
 
sasa laki 2 na nusu inatosha kulipa hasara ya magari matatu ?

nilimuona jana alivokua anawambia Trafic ni wasenge najua angekua sio mtoto wa kigogo angepata tabu sana
 
Vigogo hata bima za magari hawalipi. Kuendesha wakiwa wamelewa hawajui kuwa inakatazwa. Ama kweli hili ni kundi la walamba asali ambalo hata tozo haziwahusu.
 
Yani faini waliompiga dogo anailipa mwenyewe apo apo bila hata ya kuomba home inavyosemekana uko alipotoka kaunguza zaidi ya milioni na chenji zake
 
Kumbe inawezekana kabisa, kushtakiwa siku hiyo hiyo, kufikishwa mahakamani siku hiyo hiyo, kusomewa mashtaka siku hiyo hiyo, na kuandikiwa hukumu siku hiyo hiyo!
Ndiyo maana watu wanapodai katiba mpya hawa hushangaa kwa sababu wao si kama sisi...
Wala wao hawatendewi kama sisi... Hawapigwi virungu, na makosa makubwa makubwa yanayoweza kuwanyima dhamana hawasomewi ng'o!
 
Unadhani kabisa hatagusa gari for 6 months?? Haya vipi kuhusu lugha chafu na matusi?

That's none of my business. Hiyo ndo sheria kwa hilo kosa across the board, kama atafanya kosa tena hainihusu.
 
Daah mfanyabiashara James simbachewene hatimae kaachiwa.
 
Back
Top Bottom