Mtoto wa Simbachawene alimwa faini ya tsh. 250,000/=

Mtoto wa Simbachawene alimwa faini ya tsh. 250,000/=

View attachment 2333685
Mfanyabiashara, James Simbachawene (24) ambaye ni mtoto wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene, amehukumiwa kulipa faini ya Sh250, 000 na kufungiwa leseni yake ya udereva kwa miezi sita baada ya kukiri makossa matatu.

Mtoto huyo amefikishwa mahakamani hapo leo Jumatano Agosti 24, 2022 jioni na kusomewa mashtaka yake na wakili wa Serikali, Daisy Makakala, mbele ya Hakimu Mkazi Aron Lyamuya.

Mashitaka hayo ni pamoja na kuendesha gari kwa hatari, kuendesha gari akiwa amelewa na kuendesha gari bila kuwa na bima.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Simbachawene alikiri na ndipo hakimu Lyamuya alipoahirisha kesi ili kumwandikia hukumu.

Baada ya muda mfupi, ndipo hakimu Lyamuya alimhukumu Simbachawene kulipa faini ya Sh100,000 kwa kosa la kuendesha gari kwa hatari, Sh100,000 kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa na Sh50,000 kwa kosa la kuendesha gari bila kuwa na bima.

Pamoja na faini hiyo, leseni ya Simbachawene imefungiwa kwa miezi sita.
Credit; Mwananchi News Paper
duh... Bima ya chombo ina gharama kuliko faini yake, Nashukuru kwa kulifahamu hilo🙏
 
Traffiki ni wapuuzi sana na katika issue hii dogo nasikitika kusema mahakama imetumika vibaya ku-over-do!

Hapakua na issue yoyote ya maana pale.
 
Hivi gharama ya kukata 3rd party insurance vs fine ya kosa la kutokua na insurance ipi imekua kubwa hapo?
 
ningekuwa mimi pamoja na yote hayo, ningejiuzulu nafasi yangu niliyo teuliwa ili kuonyesha uwajibikaji kwa kitendo alicho fanya mtoto wangu haswa pale alipo tumia cheo cha Baba yake kujigamba kuwa yupo juu ya sheria na anaweza fanya makosa bila kuchukuliwa hatua kwa kutegemea wadhifa wa Baba yake.

viongozi wetu kuweni na utamaduni wa kuwajibika nyinyi wenyewe kwa makosa mbalimbali yanayo jitokeza, sio mpaka unyofolewe.
Kuonesha hasira acha hio kazi uliyonayo mkuu ili iwe kama mfano
 
Dogo ni TISI-CCM huyo, hukumu ya mchongo.
 
TZS 250,000/= kwa mtoto wa Waziri ni issue ndogo tu. Ni swala tu la Chawene Mkubwa kupiga simu moja tu hela ikaletwa fasta.
Hata yeye kwa jinsi alivyorekodiwa, alidai ana pesa, naona kulipia bima ya gari aliona sio kipaumbele.
 
Unadhani ndo hataonekana road na gari? Labda sio Tz...ataendesha vizuri tu
Mbona hata mim nna mwaka sasa sna bima wala sija update lesen. Hahah. Bonho raha sana.. natoka asubuh sa 12 hamna askar narud sa 12 jion hamna askar.. hahah

Ukitaka kamatwa toka saa nne asubuh au tembea mida ya mchana lazima askar akusimamishe
 
Traffic case ni kesi za kawaida sana hata angegonga akaua watu 10 bado adhabu yake ingekua siyo kubwa kesi za barabarani hazina mambo mengi labda uwe hauna lesen ndo inakuaga ngumu kidogo hata makosa aliyo yafanya huyo jamaa ni makosa ya kawaida tu ila kwakua ni mtoto wa kiongozi ndo maana imechukuliwa tofauti ila Sheria ni 1 tu
Ndio maana babaake kasema achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.
Alikua anajua tobo liko wapi.
Kumwambia mwanae kubali umefanya basi kaadhibiwa kwa mujibu wa sheria analipa anatoka.
 
Utapewa kesi ya Kutukana matusi, utapewa kesi ya kumzuia askari kufanya majukumu yake, na jinai zingine kadhaa tu hivi. Hiyo miezi anayofungiwa kuendesha gari lakin anakua uraiani, kama ndio wewe utakua uko mahabusu ukiwa ushakula virungu vya kutosha tu.
Vile virungu sijui vimetengenezwa na nini kwa ule mdundo wake katika ugoko na kwenye maungio ya mkono😭
 
250K , hela ya kifurushi cha DStv?
Siku zote nawambiaga watu, ukiwa unavuka barabara fanya chap usilinge. Sheria za makosa barabarani adhabu zake ni ndogo sana. Jamaa-angu aligonga na kuua Kimara, akakili kosa mahakamani alilipa 186k tu, eti gari ndo iliyoua sio yeye kwa kuendeshwa kwa uzembe.

Kwahiyo na ya huyo dogo kulipa 250k sishangai. Wenye magari yaliyoumizwa watalipwa na bima zao. Kwanza hawatasumbuliwa na milolongo ya makampuni ya bima sababu iko kwenye public demain, issue nzima
 
View attachment 2333685
Mfanyabiashara, James Simbachawene (24) ambaye ni mtoto wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene, amehukumiwa kulipa faini ya sh. 250,000 na kufungiwa leseni yake ya udereva kwa miezi sita baada ya kukiri makosa matatu.

Mtoto huyo amefikishwa mahakamani hapo leo Jumatano Agosti 24, 2022 jioni na kusomewa mashtaka yake na wakili wa serikali, Daisy Makakala, mbele ya Hakimu Mkazi Aron Lyamuya.

Mashitaka hayo ni pamoja na kuendesha gari kwa hatari, kuendesha gari akiwa amelewa na kuendesha gari bila kuwa na bima.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Simbachawene alikiri na ndipo hakimu Lyamuya alipoahirisha kesi ili kumwandikia hukumu.

Baada ya muda mfupi, ndipo hakimu Lyamuya alimhukumu Simbachawene kulipa faini ya Sh100,000 kwa kosa la kuendesha gari kwa hatari, Sh100,000 kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa na Sh50,000 kwa kosa la kuendesha gari bila kuwa na bima.

Pamoja na faini hiyo, leseni ya Simbachawene imefungiwa kwa miezi sita.

Chanzo: Mwananchi News Paper
Katukana na kudharau mamlaka, huyu ilibidi apewe hata miaka 15 jela na faini si chini ya milioni 10. Kamdhalilisha sana babake na familia yake.
 
Mbona hata mim nna mwaka sasa sna bima wala sija update lesen. Hahah. Bonho raha sana.. natoka asubuh sa 12 hamna askar narud sa 12 jion hamna askar.. hahah

Ukitaka kamatwa toka saa nne asubuh au tembea mida ya mchana lazima askar akusimamishe
Tupo wengi😃
 
Back
Top Bottom