JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Watoto wenye umri wa miaka 5 kushuka chini hawatakiwi kuvaa barakoa
Hii ni kwa sababu ya usalama na uwezo wa mtoto kutumia barakoa ipasavyo bila msaada wa mtu mzima.
WHO na UNICEF wanashauri kwamba uamuzi wa kutumia barakoa kwa watoto wenye umri wa miaka 6-11 unapaswa kuzingatia mambo yafuatayo:
Ikiwa kuna maambukizi mengi katika eneo analoishi mtoto
Uwezo wa mtoto kutumia barakoa kwa usalama na ipasavyo
Usimamizi wa kutosha wa watu wazima na maelekezo kwa mtoto juu ya jinsi ya kuvaa na kuvua barakoa
Mwingiliano wa mtoto na watu wengine ambao wako katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa Korona, kama vile wazee na wale walio na matatizo mengine ya kiafya.
Aidha inashauriwa kwamba watoto wenye umri wa miaka 12 na zaidi wanapaswa kuvaa barakoa kama watu wazima, haswa katika mazingira ambayo hawawezi kuhakikisha umbali wa mita 1 kutoka kwa wengine
Upvote
0