Mtoto wako akiamua kumpa nyumba baba/mama yake ni sahihi?

Mtoto wako akiamua kumpa nyumba baba/mama yake ni sahihi?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Huyu ni mtoto wa ujanani, kwakuwa bado wote au mmoja wenu alikuwa bado mwanafunzi wazazi wenu waliwasaidia ulezi mpaka mlipopata uwezo wa kumlea mtoto.

Mengi yalipita na nyinyi wawili hamkuoana tena. Kabla ya kuingia kwenye ndoa mpya unaamua kumnunulia mtoto wako wa kwanza nyumba. Wakati huo mtoto bado yuko shule ya upili lakini kwakuwa ni muelewa unamueleza ukweli.

Mtoto anakushauri nyumba ipangishwe ili imsaidie mahitaji yake ya maisha pamoja na shule. Unaona si wazo baya unamkabidhi mtoto nyumba ile.

Mzazi mwenzako huko amepigika kimaisha, mwanao anaamua amstiri Baba/mama yake. Hapa hawezi tena kumuondoa mpaka mauti yamfike. Hili jambo limekaaje?
 
Mtoto yupo Sekondari ya Upili,bila shaka ana miaka 18 na zaidi. Ana uwezo wa kujiamulia mambo yake.

Kwa kuwa ni mzazi wake basi akae naye. Najaribu kujiweka nafasi ya endapo mimi ndiye mzazi niliyepigika na maisha. Bila shaka ningeshukuru kupata pa kujisitiri.
 
Kama umeshamkabidhi mtu kitu, kitu hicho kinakua mali ya huyo uliemkabidhi na kuanzia hapo yeye ndio anakua na maamuzi juu ya kitu hicho. Unless uwe umemuazimisha kwa muda, au umempa masharti ya jinsi unavyotaka kitu hicho kitumike.
 
Back
Top Bottom