Mtoto wangu ana baba wawili

Mtoto wangu ana baba wawili

Kapime DNA upate uhakika, kwa wanawake wa sasa inawezekana hata nyie wote wawili mtoto sio wenu.
Nimecheka sana hii comment, hapo umemkatisha matumaini muhusika moja Kwa moja.!

Nasikia ukienda kupima DNA lazima waseme mtoto ni wako ili kuweka mambo sawa.

Nafikiri alee tu so longer anafanana na hesabu zimethibitisha n wake haina shida.
 
Wakuu maisha yangu yamejaa mapito magumu sana ambayo kuwa sitarajii kabisa kukutana nayo kwenye maisha yangu.

mwaka juzi mwezi wa kumi tarehe 9 nilitoka mbeya na kurudi dar na kesho yake nilikutana kimwili na mwanamke ambaye tulikuwa na mahusiano kitambo . Baada ya kumaliza yaliyonileta dar nilirudi kwenye harakati za mikoani . Baada kama ya mwezi yule mwanamke aliniambia ameshika ujauzito mimi nilifurahi ila nikawa na wasiwasi huenda mimba sio yangu.

Nikamjulisha hilo akadai kuwa ni uhakika mimba ni yangu . Nikamjulisha basi kama mimba ni yangu lazima ajifungue tarehe 10 mwezi wa saba mwaka jana.

Na kweli alijifungua tarehe hiyo hiyo nilikuwa nisharudi dar na nilimhudumia vizuri tu japo sio kwa ukubwa ambao ningemhudumia kama nisingekuwa na mashaka.

Naomba niwajulishe zaidi kuhusu huyu mwanamke. Alikuwa na mtoto mmoja alizaa na jamaa mmoja . wakati nipo kwenye mahusiano nae nikiwa dar alikuwa kwa wazazi sikuwa nimepata taarifa kuwa tayari alienda kuishi na jamaa.

Sasa mwaka jana mwezi wa 12 nikawa nimepigiwa simu na namba ngeni nikapokea . Baada ya salamu jamaa akaniuliza unamfahamu Rose ( sio jina halisi)

Nikamjibu ndio namfahamu

Ninani kwako . Nikamjibu kwanini unaniuliza

Ndio akaniambia kuwa amekuwa akiona mawasiliano yangu na rose mda mrefu ila kuwa hajui kinachoendelea na muda mrefu anaishi na rose.

Nikaamua kumuuliza mtoto wa mwisho niwa kwako akadai ni wake aisee?

Moyo ulishtuka sana?

Ikabidi nimwambie ukweli kuwa ni mtoto wangu na nipo kwenye mahusiano na rose kitambo kumwaminisha zaidi ni cheti cha kuzaliwa cha mtoto ambacho kina jina langu na jina nililompa mtoto mimi
Japokuwa baadae niligundua nyumbani kuwa wanamwita jina jingine

Basi jamaa tulitulizana kiume na akadai kwenda kupima DNA ila jioni yake nikampigia akiwa na rose nikamwambia ampe simu rose aweke loud speaker aseme mtoto ni wanani ila rose aligoma katu , tukapanga tutakutana tuongee na jamaa ila akapotea moja kwa moja na alinyamaza.

Mahusiano yao yaliyumba akamwacha mwanamke mwenyewe mpaka sasa anafika mara chache sana na hahudumii kama awali na mimi vivyo hivyo nimepunguza sana kuhudumia.

Japokuwa ananiaminisha sana na mtoto ana vingi anafanana na mimi zaidi ila mashaka yapo . Hata wazazi wake aliwaambia mtoto Mtoto ni wangu ila bado hata nao siwaamini sijui nifanyeje moyo wangu uwe huru

Ni mtoto kike mzuri sana.

Natamani sana hili likae vizuri.

Kama ni mtoto wangu nimpe matunzo asilimia mia na nimweke moyoni nifurahie.

Kama sio mwanangu basi ni move on.

Hili linaniumiza sana maana sina ujasiri wa kukemea malezi anayolelewa mwanangu na ningependa kuandaa future yake nimfungulie account mapema nianze kumwekea vishilingi lakini ndio hivyo nipo katikati

Mnanishauri nifanyeje wakuu?
Ukitaka kujua ukweli, tishia kama unataka umchukue mtoto akalelewe na bibi yake yaani mama yako uone, akiruhusu huyo mtoto n wako, akigoma basi jua siku ulipompitia wewe next day akaenda kudaka Kwa mwingine
 
Nishamtishia DNA wala hata hawazi na anajua nina kipato kikubwa tu cha kumudu
 
Nimecheka sana hii comment, hapo umemkatisha matumaini muhusika moja Kwa moja.!

Nasikia ukienda kupima DNA lazima waseme mtoto ni wako ili kuweka mambo sawa.

Nafikiri alee tu so longer anafanana na hesabu zimethibitisha n wake haina shida.
Duuh ndivyo ilivyo tena laki tano wanaila kiwepesi hivyo
 
Mnapendaga tu kutusimulia yaliyowakuta...Sasa ndio swali Gani Hilo?
 
Kam ulipg hesabu za mtoto kujifung Tareh x mwez x na ikawa bas n wako

NO 2. Kafanye DNA za kienyeji
Kwenye DNA za kienyeji awe makini asije ongeza mlemavu kwenye jamii
 
Wakuu maisha yangu yamejaa mapito magumu sana ambayo kuwa sitarajii kabisa kukutana nayo kwenye maisha yangu.

mwaka juzi mwezi wa kumi tarehe 9 nilitoka mbeya na kurudi dar na kesho yake nilikutana kimwili na mwanamke ambaye tulikuwa na mahusiano kitambo . Baada ya kumaliza yaliyonileta dar nilirudi kwenye harakati za mikoani . Baada kama ya mwezi yule mwanamke aliniambia ameshika ujauzito mimi nilifurahi ila nikawa na wasiwasi huenda mimba sio yangu.

Nikamjulisha hilo akadai kuwa ni uhakika mimba ni yangu . Nikamjulisha basi kama mimba ni yangu lazima ajifungue tarehe 10 mwezi wa saba mwaka jana.

Na kweli alijifungua tarehe hiyo hiyo nilikuwa nisharudi dar na nilimhudumia vizuri tu japo sio kwa ukubwa ambao ningemhudumia kama nisingekuwa na mashaka.

Naomba niwajulishe zaidi kuhusu huyu mwanamke. Alikuwa na mtoto mmoja alizaa na jamaa mmoja . wakati nipo kwenye mahusiano nae nikiwa dar alikuwa kwa wazazi sikuwa nimepata taarifa kuwa tayari alienda kuishi na jamaa.

Sasa mwaka jana mwezi wa 12 nikawa nimepigiwa simu na namba ngeni nikapokea . Baada ya salamu jamaa akaniuliza unamfahamu Rose ( sio jina halisi)

Nikamjibu ndio namfahamu

Ninani kwako . Nikamjibu kwanini unaniuliza

Ndio akaniambia kuwa amekuwa akiona mawasiliano yangu na rose mda mrefu ila kuwa hajui kinachoendelea na muda mrefu anaishi na rose.

Nikaamua kumuuliza mtoto wa mwisho niwa kwako akadai ni wake aisee?

Moyo ulishtuka sana?

Ikabidi nimwambie ukweli kuwa ni mtoto wangu na nipo kwenye mahusiano na rose kitambo kumwaminisha zaidi ni cheti cha kuzaliwa cha mtoto ambacho kina jina langu na jina nililompa mtoto mimi
Japokuwa baadae niligundua nyumbani kuwa wanamwita jina jingine

Basi jamaa tulitulizana kiume na akadai kwenda kupima DNA ila jioni yake nikampigia akiwa na rose nikamwambia ampe simu rose aweke loud speaker aseme mtoto ni wanani ila rose aligoma katu , tukapanga tutakutana tuongee na jamaa ila akapotea moja kwa moja na alinyamaza.

Mahusiano yao yaliyumba akamwacha mwanamke mwenyewe mpaka sasa anafika mara chache sana na hahudumii kama awali na mimi vivyo hivyo nimepunguza sana kuhudumia.

Japokuwa ananiaminisha sana na mtoto ana vingi anafanana na mimi zaidi ila mashaka yapo . Hata wazazi wake aliwaambia mtoto Mtoto ni wangu ila bado hata nao siwaamini sijui nifanyeje moyo wangu uwe huru

Ni mtoto kike mzuri sana.

Natamani sana hili likae vizuri.

Kama ni mtoto wangu nimpe matunzo asilimia mia na nimweke moyoni nifurahie.

Kama sio mwanangu basi ni move on.

Hili linaniumiza sana maana sina ujasiri wa kukemea malezi anayolelewa mwanangu na ningependa kuandaa future yake nimfungulie account mapema nianze kumwekea vishilingi lakini ndio hivyo nipo katikati

Mnanishauri nifanyeje wakuu?
• Da pole sana aise... ☹️☹️,

• Nipo kwenye sekeseke kama lako hili, now kesi ipo mahakamani...

• Mahakama nimeigomea kuwa siwezi kulea mtoto , mpaka tupime DNA kwanza.....
 
Back
Top Bottom