Mtoto wangu anayeishi na mama yake tulieachana analelewa ndivyo sivyo, ustawi wa jamii imeshindikana kumchukua, mama yake hataki niwe nae, nifanyeje?

Nibora ukamwacha hukohuko kwa mama yake
Mana pamoja na changamoto ya mama yake lakini bado ni bora kuliko huyo mkeo mpya
 
Kina junior ndio walivyo lakini pia wanawake wengi wananufaika na hela wanazotuma wanaume za matunzo hvyo hawezi kubali umchukue.
 
Hapo utumie akili usikurupuke, huyo mtoto anaweza lishwa sumu na mama yake mbele ya safari akaenda kuongea uongo ilimradi usiishi nae, na mtoto kama ndio huyo wa kupenda chipsi mayai kila siku hawezi kuondoka kwa mama yake kirahisi.

Tumia akili hasa kutengeneza urafiki wa karibu na mama yake, piga nae story sana kila siku ili ukija kumwambia habari za kumhamishia mtoto shule za mjini kwa manufaa yake ya baadae, uekeweke, issue itakuja mama yake anaweza kujiweka pembeni kumsomesha, hiyo kazi itakuwa yako.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Pagumu hapo hao wanawake huwa wamesoma shule gani za kukufundisha kumlisha mtoto junk foods kila siku?
Ukitamka kumchukua mtoto nadhani utakuwa ugomvi muhimu tenga mda wa likizo uwe unakaa naye na kumfundisha baadhi ya namna mwanaume anatakiwa kuwa ,kama njia hiyo haitafanya kazi angalia namna ingine(nadhani mwanamke wako hatokataa akae kwako likizo)
Swali langu ni je huyo mkeo wakati unamuoa ulimficha kuwa una mtoto?
 
Hata mi nimeshangaaa,
 
Hiyo Sheria ya miaka saba inatoka wapi? Binti yangu nilimchukua kwa mama yake akiwa na 4yrs. Nafikiri ustawi wanaangalia zaidi wapi mtoto atalelewa vizuri
 
Tatizo sio mama yake Wala usitawi wa jamii, Bali ni wewe kukosa sifa za uanaume.
Wakati unaoa mke mwingine hakutakiwa kukupa sharti la kukataa kukaa na mtoto wako. Kama alikupa na wewe ukakubali ni wazi amekutawala kwani mtoto ulimpata kabla ya kukutana naye.
Kama ungechukua nafasi yako Kama mwanaume haya yasingetokea.
 

Achana na huyo mtoto ishi kwa Amani, utanishukuru baadae.
 
Sonma kwa utulivu mada ndiyo utoe maoni yako, ili kuepuka aibu ndogondogo kama hizi !
 
Fosi uishi na mwanao,kama mkeo hataki aondoke yeye.
 
Kachukue mwanao akileta ngebe mtengenezee mwanya mdomoni mwake kwa ghafla.
 
Jifanye bogas kumbe una lako ...panga namna ya kumuiba na mpeleke mbali kwa ndugu na ukimhiba waambie nimeshachukua dam yangu msihangaike kumtafuta.
 
Jizime data mchukue muelimishe mke tafuta watu wamuandae mke kisakolojia
 
Athari za wazazi kutengana. Una uhakika ukimchukua wewe atapata malezi bora kutoka kwa mama yake wa kambo?
Binadamu wabinafsi hapo anajua mtoto hata amchukue atapata tabu , mda huo ana mwanamke wmingine ambaye atamtesa ...Huu ndio ujinga wa kuzaa ni kumkatili mtoto .

walioachana washapata wenza ila mtoto hawezi kupata malezi mazuri milele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…