Mtu abisha hodi mchana, kwanini umuulize "wewe ni nani"?

Mtu abisha hodi mchana, kwanini umuulize "wewe ni nani"?

Restless Hustler

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2017
Posts
5,150
Reaction score
20,025
Habari za muda huu!

Mtu anabisha hodi mchana kweupe, kwanini umuulize "wewe ni nani"?! Sioni mantiki ya kumuuliza hili swali mchana. Ingekuwa ni usiku sawa maana usiku una mambo mengi.

Binafsi nikigonga mlango mchana, mtu aniulize hivyo huwa natafsiri kwamba ni dalili ya ubinafsi na ni upungufu wa upendo. Wewe mdau wa JF unatafsirije hicho kitendo?!
 
Utakuja kudhuriwa na kujifanya kwako kuwa una upendo na sio mbinafsi. Yani mtu agonge geti au mlango nisiulize nani eti kisa ubinafsi sijui nakosa upendo, hali ya sasa sio salama ni vyema kujiridhisha kabla.
Tz Kuna Amani. Japo Kuna kipindi utekaji ulishamiri but we are back to normal.
 
Kwani hujawahi kuskia watu wanavamiwa au kuawa mchana wakiwa kwenye makazi yao?
 
Tz Kuna Amani. Japo Kuna kipindi utekaji ulishamiri but we are back to normal.
Amani ya wapi, kila leo vibaka wanaruka ukuta wanakwapua hadi malapa watu hawako kama unavyowafikiria ni muhimu kujua ni nani anabisha hodi iwe mchana hata usiku. Tena kama usiku ndo sifungui hadi niwe na hakika ni nani anaebisha hodi.
 
Back
Top Bottom