Mtu akifa anaenda wapi?

Alipomwambia yule muuaji msalabani, Leo hii utakuwa nami Mahali pema peponi, unaamini huko peponi hawatambuani?
Kwa nini siku mbili baadaye, wakati wa ufufuo, Yesu akathibitisha kwamba hakuwa amepaa kwenda kwa Baba (Yohana 20:17)?

Au huko peponi ni wapi asipokuwepo Baba?

Musa na Elia walipomtokea Yesu mlimani wakimtia moyo, ulidhani yalikuwa maigizo Yale?
Kwa maelezo yako, alikuwepo Eliya (mwili na roho) na Musa (roho)? Maana Eliya yeye hakufa.

Kwa taarifa Yako, Musa na Elia na Manabii wote wa AGANO la kale wa Mungu, wapo Mbinguni,
Kulikuwa na sababu gani basi ya manabii kama akina Ayubu, Danieli na kadhalika kutazamia siku ya ufufuo kama tumaini lao pekee?

Maana kama roho iko mbinguni tayari, kwa nini wasingeshangilia kwamba mara tu baada ya mauti yao wangeonana na Mungu uso kwa uso?

WATAKATIFU wote wafao katika Mungu baada ya kufufuka Yesu, wako Mbinguni. Hawakai tena Mahali pa kusubiri.
^Strange fire!^

MTU ni ROHO, anayo NAFSI na anaishi ndani ya MWILI.

Mtu Hafi, anabadili form, mwili ndio unaokufa na kuoza,
^Strange fire!^

Mtu aliumbwa kuishi milele,mtenda dhambi ukifa(ukibadili form) utateswa milele, mtakatifu ukibadili form( ukifa) unafurahia maisha milele.
^Strange fire!^

kuzaliwa duniani ni bahati hasa kuzaliwa binadamu so ishi dunia hapa ndo peponi hakuna sehemu utaenda ukifa zingne story za vijiweni
Kama hakuna ufufuo, kuna bahati gani kuwepo duniani? Mbona unajichanganya?

Maisha yana chanzo na kusudi.

Au uniambie mwanadamu chanzo chake nini? (Tuchukulie kwamba Mungu hayupo).
 
Lazima uwe na upeo mkubwa kidogo kuelewa dunia pia sio wote mtaielewa dunia
 
hakuna NAFSI, hakuna ROHO,...kama vingekuwepo, basi tungelikuwa na kumbukumbu ya wapi tulikuwepo kabla HATUJAZALIWA...kwa ufupi hizo ni stori tu za kuendelea kuwashika WAJINGA...kule anakoenda Sisimizi au Mbuzi baada ya kufa ndiko mwanadamu aendako pia, mwanadamu huna u-special wowote zaidi ya kuwazidi viumbe wengine UJINGA tu...
 
Elia hakufa, Musa alikufa,

Nami nikuulize, ikiwa ukifa habari ndio inaishia pale,

Waliokuwa wakiongea na YESU mlimali ni akina nani?
 
Usizidiwe Maarifa na wachawi,

Ikiwa Roho na NAFSI hazipo, wachawi hutumia nini kupaa angani, wanawezaje kutumia ungo mmoja kukaa watu zaidi ya 20 na wakasafiri bila shida yoyote?

Mtafute Mungu, tafuta Maarifa, utakuwa msindikizaji na mtumwa wa Ibilisi Hadi lini?
 
Unaweza nilitea picha ya wachawi 20, wakiwa kwenye ungo?......Munaweza kupaa na ungo tu,ila bado munatibiwa maralia kwa msaada wa watu wa Marekani..?..

WAAFRIKA ACHENI IMANI ZA KIPUMBAVU....
 
Unaweza nilitea picha ya wachawi 20, wakiwa kwenye ungo?......Munaweza kupaa na ungo tu,ila bado munatibiwa maralia kwa msaada wa watu wa Marekani..?..

WAAFRIKA ACHENI IMANI ZA KIPUMBAVU....
Kazi ipo
 
Unaweza nilitea picha ya wachawi 20, wakiwa kwenye ungo?......Munaweza kupaa na ungo tu,ila bado munatibiwa maralia kwa msaada wa watu wa Marekani..?..

WAAFRIKA ACHENI IMANI ZA KIPUMBAVU....
Nenda kamuulize mama Yako alipokuzaa, kitovu chako alipokikata alikitunza wapi ndipo uje useme Ulimwengu wa Nuru na Giza ni story!!

Siku utakapolala umefunga milango na ukaamka uko kwenye majaruba ndio utajua uchawi upo au la!!

Ndio ninyi mnaenda shule Kisha mnamkataa hata Mungu na kuzidi kutokomea gizani kuliko kupata Nuru.

Sorry Kwa lugha ngumu!!
 
Ni vigumu kujua kwa sababu waliokufa hawajawahi kurudi ili watujulishe walikoenda, ila labda tukuue wewe unayetaka kujua, ukipenda japo si lazima urudi kutujulisha ulikuwakuta wenzako.
 
Hili jambo nimewahi kujiuliza. Binadamu ana utofauti upi na viumbe wengine? Kwanini masuala ya mbinguni hayahusishi ng'ombe, vyura na viroboto?

Jibu ni kuwa ukishasema mambo ya kwenda mbinguni umehusisha masuala ya imani, imani ya binadamu sio ya ng'ombe.

Ila kama utaondoa mambo ya imani, hakuna tofauti yoyote kati ya mwanadamu na viumbe wengine zaidi tu kuwa binadamu ubongo wake una uwezo mkubwa kuliko wa wanyama kama ambavyo ubongo wa nyani ulivyo na uwezo mkubwa kuliko wa bata.
 
Ndo akili zenu WAAFRIKA, upumbavu tu, ndo maana mzungu alipowaachia Dini tu akamaliza kila kitu, munahangaika na vitovu ilihari munanuka umasiki wa kutupa,kitovu kina maana na kazi gani tena ilihari Kazi yake ilishakwisha baada ya mtu kuzaliwa,
Tumieni basi hayo maimani yenu ya kipumbavu kuleta maendeleo munabaki munabung'aa macho tu....

Hivi munapata wapi hata muda wa kudanganyana kuhusu maisha baada ya kifo wakati, maisha ya hapa DUNIANI tu yamewashinda, munaishi kama wanyama?...
 
Na tuumbe mtu Kwa Mfano wetu.

Mtu ni mfano wa Mungu,

Mtu ni ROHO, alitoka Kwa Mungu ambaye ni ROHO.

Akili na uwezo wa uwezo wa kufanya maamuzi,ndicho kinamtofautisha mtu na mnyama.

Mtu ni WA milele,
 
Jibu hoja. Acha kujificha kwenye kichaka cha karanga.
Sasa nishajua mtu huna upeo ni kujibu while najua huta elewa ni kupoteza muda..... kuwa msomi/mwerevu ni pamoja na kujua unabishana kihoja na mtu wa aina gani .....kama mjinga mwambie asipolewa achana nae ...ila kama mpumbavu achana nae maana kiswahili mtu mpumbavu ni yule hata ukimwambie hawezi elewa
 
hizi imani zinawafanya watu kuwa matahira sasa,.hili BARA lina watu wapumbavu sijawi ona....yani ni Binadamu tu ndo uwe na nafsi mara ROHO.., ila viumbe vingine havina?...
 
Na tuumbe mtu Kwa Mfano wetu.

Mtu ni mfano wa Mungu,

Mtu ni ROHO, alitoka Kwa Mungu ambaye ni ROHO.

Akili na uwezo wa uwezo wa kufanya maamuzi,ndicho kinamtofautisha mtu na mnyama.

Mtu ni WA milele,
According to imani upo sahihi.
 
Na tuumbe mtu Kwa Mfano wetu.

Mtu ni mfano wa Mungu,

Mtu ni ROHO, alitoka Kwa Mungu ambaye ni ROHO.

Akili na uwezo wa uwezo wa kufanya maamuzi,ndicho kinamtofautisha mtu na mnyama.

Mtu ni WA milele,
Ikiwa mtu ni wa milele maana yake pia alikuwepo hata kabla hajazaliwa, na pia atakuwepo hata baada ya kufa....

sasa wewe una kumbuka ulikuwa wapi kabla hujazaliwa?...
 
hizi imani zinawafanya watu kuwa matahira sasa,.hili BARA lina watu wapumbavu sijawi ona....yani ni Binadamu tu ndo uwe na nafsi mara ROHO.., ila viumbe vingine havina?...
Hili bara la kijinga sana mkuuu werevu kama wewe au mimi ni wachache mno ....wakutafuta na tochi.....
 
hizi imani zinawafanya watu kuwa matahira sasa,.hili BARA lina watu wapumbavu sijawi ona....yani ni Binadamu tu ndo uwe na nafsi mara ROHO.., ila viumbe vingine havina?...
Ukifata imani ndivyo ilivyo. Ila ukiiweka imani pembeni wewe na kunguni hamna tofauti. Mpo duniani kula, kunya na kufa, mengine mbwembwe.

Hata hivyo, Nje ya imani ubongo wa binadamu kupitia sayansi unafanya kazi kwa upekee sana. Pengine ukaja na dawa ya kutokufa huko mbeleni.

Nje ya imani wewe ni nani?

Wewe ni kumbukumbu ya yale uliyofanya na yale uliyofanyiwa na wengine.

Hizo kumbukumbu zimebebwa na mashine iitwayo mwili yenye kifaa maalum kiitwacho ubongo.

Sasa siri hapa ni namna ya kuzihamisha hizo kumbukumbu kwenye vifaa visivyoharibika au vifaa vingine tofauti na mwili au kuhakikisha kile kinachochakaza mwili hakichakazi.

Wanasayansi wapo kazini. Wameshafanikiwa kiasi kwenye uchakavu wa umbile la nje yaani sura. Sasa hivi ukiwa na pesa unaweza kuwa na miaka 60 ila ukaonekana kama una upo 20's.

Tunavyojadili hapa kuna program za kulipia za kugandisha mwili ikiaminika kwamba miaka mingi mbeleni tech itakuwa imekuwa juu kiasi cha kuurudisha mwili hai tena, hivyo si lazima uzikwe ukiwa na pesa, unaweza lipia ukagandishwa kwa vifaa maalum. Au kama ni mgonjwa na sasa hakuna dawa unaweza lipa ukasubiri miaka 200 ijayo dawa ikipatikana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…