Mtu akifa anaenda wapi?

Nani anajua?,hakuna aliyerudi kutupa jibu , ukienda umeenda
 
Ulichokifanya,ni kulazimisha Biblia ifuate akili yako inavyotaka kadiri ya matakwa ya Imani yako.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Ninacho weza kusema nikua umechagua kua mpumbavu. hakuna ushahidi wowote unathibisha uwepo wa Adam Hawa Wala abil Wala kaini
 
kwasababu nilizaliwa.... simple
I mean,.. kwanini unazaliwa, unaishi kisha unakufa?

Je, maisha yetu hapa Duniani hayana mantiki yoyote inayofanya yawe meaningful?
 
Una ushahidi gani kwamba kuna mungu, ahera,paradiso, na jehanamu? au unaleta hadithi za kusadikika
 
Hizi zote ni hadithi tu,

Hakuna mtu anaweza thibitisha hayo.

" Wote wanaosema kuwa kila kitu kimepangwa na Mungu na hakuna kitu unaweza fanya kubadilisha,

Nenda uwaangalie walivyo makini kabla ya kuvuka barabara. "
 
Katika kipindi cha Elisha kulikuwa na wenye ukoma wengi katika Israel ila ni Naamani pekee aliyetakaswa wakoma wengi walikufa na ukoma wao kwa hiyo imani yako ndio itakayokuponya au kukuangamiza. Haijalishi unaamini life after or not
Pamoja na kuita kundi flani kuwa ni washenzi,
Kwa kutokujua tu usahihi wa mambo (upotofu)

Naomba unijibu maswali haya matatu

1) Maybe sjakuelewa tu, Unamaanisha nini unaposema kuwa "you can not change the reality of life after death" .

2) Is it possible for living organism to have life after death?

3) Unaelewa kifo ni nini!?
 
Zaburi 73:17 ukianzia mstari wa kwanza kabisa utaona mtazamo wa Daudi juu ya hatma ya wenye kiburi aliielewa vema pale alipoamua nanukuu

17 "Mpaka nilipoingia mahali patakatifu pa Mungu penye utukufu, Nami nikatambua wakati wao ujao. " Kuna mambo hutayajua mpaka umeamua kuyajua ila ukibaki na ubishi hutoelewa baadhi ya mambo japo yapo.
 
Ukweli ni kuwa sote tunaopumua ni viumbe hai ila mwanadamu ni level nyingine Yesu anasema katika kitabu cha
Luka 12:6S hore watano huuzwa kwa sarafu mbili za thamani ndogo, sivyo? Na bado Mungu hamsahau hata mmoja. 7 Lakini hata nywele zote za vichwa vyenu zimehesabiwa. Msiogope; ninyi ni wenye thamani kuliko shore wengi.

Viumbe wengine Mungu alitupa wanadamu tuvitawale na vingine kama vitiweo tu havina future na ukirudi kwenye bustani ya Eden kabla ya anguko sote tulikuwa sawa maana tulipaswa kuishi milele na wanyama wote wangeishi milele ila kinyama zaidi bila ya mavazi.
Swali linakuja kwa nini wanyama wanakufa wakati hawakushiriki dhambi?. Jibu ni kuwa dhambi ilikusudia uharibifu kwa viumbe vyote kupitia magonjwa kisha kifo viumbe vyote vinakufa ili usalama uwepo ie. Vile vilivyo dhaifu kutokana na madhara ya dhambi lazima viondoke kuhifadhi vyenye nguvu.

Kifo ni adhabu aliyopewa mwanadamu ili asiendelee kukaa katika mwili ni madhara ya dhambi na ndio maana hakuna kifo kizuri vyote usababishwa na magonjwa, ajali n. K.
Mauti au kifo au vifo vipo vya aina mbili Kimaandiko.

1. Roho kuacha mwili

Mathayo 10:28 Na msiwaogope wale wanaoua mwili lakini hawawezi kuua nafsi; badala yake, mwogopeni yule anayeweza kuangamiza nafsi na mwili katika Gehena
2.Roho kutengwa na muumba wake

Ufunuo 20:14 Na kifo na Kaburi vikatupwa ndani ya lile ziwa la moto. Hilo linamaanisha kifo cha pili, lile ziwa la moto. 15 Zaidi ya hayo, yeyote ambaye hakupatikana ameandikwa katika kile kitabu cha uzima alitupwa ndani ya lile ziwa la moto. Asante karibu kwa maswali zaidi.
 
Nmekuuliza swali zuri na lenye kueleweka,

Wewe unaleta mahubiri
 
Utanijibu ipasavyo nlichokuuliza?
 
Unataka majibu Gani Sasa nje ya
Nmekuuliza swali zuri na lenye kueleweka,

Wewe unaleta mahubiri
Injili?. Ila linatimia NENO " injili kwa wanaopotea ni upuzi bali kwetu sisi tuokolewao ni nguvu inayoleta wokovu".
 
Unataka majibu Gani Sasa nje ya

Injili?. Ila linatimia NENO " injili kwa wanaopotea ni upuzi bali kwetu sisi tuokolewao ni nguvu inayoleta wokovu".
Rejea post #69,

Hapo ndo maswali yangu yalipo

Jibu kwa ku quote swali moja badala ya jingine.

Mahubiri hayafanyi kazi hapo

Zaidi ya kwamba utaendelea kuonesha kuwa imani ni shambulio la akili kiasi cha wewe kushindwa kujibu maswali kwa ustadi.
 
Nimedandia tu

1. Je, kuna mwisho wa dunia?

2. Waliotupwa kwenye ziwa la moto watafufuliwa siku ya mwisho

3. Katika dalili zilizotajwa kwenye vitabu vya dini.. mwisho umekaribia au bado?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…