Mtu aliyejitoa tayari kwenye Uchaguzi anakuwaje Threat kwako. Kwanini uhangaike nae?

Anonymous Caller

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2016
Posts
1,434
Reaction score
1,930
Mshindani aliyejiondoa kwenye Uchaguzi ujao, kwa lugha ya kisasa mnasema "ameweka mpira kwapani"
Yanini akusumbue.....kwanini usiachane nae?

Kwasababu amekuwa si mshindani wako tena.

Naomba niwe straight tu.
CCM kwenye uchaguzi ujao ina mteremko.....nasema hivi nikiamini uchaguzi lazima utafanyika..

Sasa hofu inatoka wapi hadi wateke watu, wapoteze watu, wapige watu, waue watu, waweke watu vizuizini nk
Kwanini?

Uchaguzi ujao CCM ndiye tume, ndiye msimamizi wa uchaguzi, yeye ndiye wakala, sasa nguvu za nini.

Kamati kuu ya CHADEMA ilipendekeza kwamba uchaguzi usogezwe mbele hata miaka miwili au mitatu mbele..
Ili kupisha marekebisho ya sheria..

Kwenye hiyo break, serikali iliyopo iendelee kuongoza......sasa hilo nalo wanakataa! Wakati wanaendelea kuongoza dola.......shida ipo wapi.....kama wewe ni mbunge utaendelea na ubunge wako.....kama ni waziri...utaendelea na uwaziri wako....kama ni Rais ni hivyohivyo..
 
Kwani wanahangaika Mkuu?
 
Mchezo mtamu adui akiwa uwanjani bana asikwambie mtu....

akiwa nje hata ukishinda unakuwa huna raha na ushindi.
 
Ndio hapa naona wanasiasa wa Tanzania kuna IQ ndogo tu. Mfano kama unajua utaiba kura kuna haja gani ya kuzuia mikutano au kubambikia watu kesi za uhaini ilihali uchaguzi ukifika utaiba tu?

Hata JK aliiba uchaguzi wa 2010 ila hakuzuia mikutano wala kuwapa watu kesi za uhaini. Ila tokea 2016 jamaa hata wakipora viti vyote bado wataua na kuteka unashindwa kuelewa wanachotaka ni nini haswa.

Lawama zote kwa Mabeyo, alikua na kazi moja tu, yaani moja tu!!
 
Ccm must out
No reform no election ⚒️ 💯
 
Na itakuwa ni ujinga wa kiwango cha juu kwa mtu yoyote kwenda kupiga kura wakati CCM imeshasema itatangazwa kushinda kwa 99%. Hata kwa mwanaccm kwa nini upoteze muda wako kwenda kupanga foleni kupiga kura ilhali wagombea wote wa CCM watatangazwa kushinda kwa 99%?
 
Labda Mabeyo na wenzake waliamini kwamba watamdhibiti na kwamba atakuwa royal kwa miongozo aliyopewa!
FUNZO: Binadamu sio wa kumkadiria kwa macho!
 
Hofu nao ni ugonjwa!
 
Ndio maana sisi tunasema no election maana yake uchaguzi usifanyike kabisa💯
 
Nchi huongozwa kwa sheria ukikosea maamuzi unaburuzwa mahakamani
 
Kwenda kuchagua makenge

Wizara ya afya iliyesha ufahamisha uma kati ya watu 4 mmojawapo ana tatizo la afya ya akili vile vile wabungu 4 kati yao kuna mmoja mwenye tatizo la afya ya akili yaani kenge
 
Ni huzuni tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…