ni miongoni mwa makosa makubwa sana kumtupa mzazi wako, hata kama huyo mzazi mlikuwa hampatani kabisa lakini unatakiwa umhudumie hata kama humpendi. ukimtupa mzazi wako kuna uwezekano mkubwa ukapata laana na hii ni kweli.
QURAN 17:23-25
23. "Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima. Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu (wazazi wangu) kama walivyo nilea utotoni. Mola wenu anajua kabisa yaliyo nyoyoni mwenu. Ikiwa nyinyi mtakuwa wema, basi hakika Yeye ni Mwenye kuwasamehe kwa wanao tubia kwake."
Kama ni muislamu huyo aliemuasi mzazi wake, kwanza kabisa amuombe Mwenyezi Mungu msamaha kwa makosa hayo, hapa itambidi aamke usiku kuswali na ajutie kabisa makosa yake hayo.
Pili awaombee dua mara kwa mara hao wazazi au mzazi aliye fariki, na awatolee sadaka, sadaka hii unaweza kuwapa yatima au masikini au kuchangia ujenzi wa msikiti n.k
Na tatu awasaidie au awe karibu na ndugu za wazazi wake ambao wao hai kwa sasa, yani asiwatupe hao ndugu za baba au mama yake.
Hii inaweza kusaidia kupunguza laana au kuiondosha kabisa kama Mwenyezi Mungu atamkubalia toba yake. (Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi)