Mtu aliyekataa kumuhudumia Mzazi wake hadi anakufa, je, afanye nini ili laana imuepuke?

Mtu aliyekataa kumuhudumia Mzazi wake hadi anakufa, je, afanye nini ili laana imuepuke?

Mungu mkuu husamehe 7 x 70...amuombe msamaha wake wa pili atasamehewa tu
 
ni miongoni mwa makosa makubwa sana kumtupa mzazi wako, hata kama huyo mzazi mlikuwa hampatani kabisa lakini unatakiwa umhudumie hata kama humpendi. ukimtupa mzazi wako kuna uwezekano mkubwa ukapata laana na hii ni kweli.

QURAN 17:23-25

23. "Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima. Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu (wazazi wangu) kama walivyo nilea utotoni. Mola wenu anajua kabisa yaliyo nyoyoni mwenu. Ikiwa nyinyi mtakuwa wema, basi hakika Yeye ni Mwenye kuwasamehe kwa wanao tubia kwake."


Kama ni muislamu huyo aliemuasi mzazi wake, kwanza kabisa amuombe Mwenyezi Mungu msamaha kwa makosa hayo, hapa itambidi aamke usiku kuswali na ajutie kabisa makosa yake hayo.

Pili awaombee dua mara kwa mara hao wazazi au mzazi aliye fariki, na awatolee sadaka, sadaka hii unaweza kuwapa yatima au masikini au kuchangia ujenzi wa msikiti n.k

Na tatu awasaidie au awe karibu na ndugu za wazazi wake ambao wao hai kwa sasa, yani asiwatupe hao ndugu za baba au mama yake.

Hii inaweza kusaidia kupunguza laana au kuiondosha kabisa kama Mwenyezi Mungu atamkubalia toba yake. (Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi)
Sahihi
 
Hakuna laana yoyote Ile hizo ni fikra potofu tu binadamu tu nadanganywa. Kafa yeye hujamuua nakumsaidia mtu au kutokumsaidia ni uamzi wako nahakuna kitakachokupata hata usipowasaidia
Una akili kweli?hujui kama kuna wakati mama yako alikuwa hapati usingizi kwa ajili yako?au alikuwa akipata chakula kidogo anaona heli alale njaa wewe ule?ogopa sana laana hasa kwa mzazi wa kike
 
Laana ni Nini ?

Hakuna Laana wewe mwenyewe ndio unaji-laani ndio maana Chizi au mtu asiyejali laana hazimpati (Dua la Kuku; as they say)

Ila wewe ukiamini kwamba kuna laana kila unalofanya unakuwa unaji-second guess; kwamba huenda hili halijafanikiwa sababu ya mzazi wangu kunilaani... Ukizingatia confidence ni kitu muhimu sana katika shughuli zako za kile siku, kwa kukosa kwako confidence mambo yako yatakwenda Kombo...

Ushauri fanya kile unachoona wewe ni sawa, ili kwa matokeo yoyote usijilaumu... (Ndio maana wafanya mabaya wengi huwa wanaji-convince kwamba tunafanya for a good cause) Yaani hata wanajeshi wanavyobaka wanawake na kuua watoto wanajipa moyo kwamba wale sio watoto wala wanawake bali na wanyama na mashetani na tunafanya kazi ya nchi...
Mpaka anakuwa chizi tayari ni laana unataka impate laana ipi tena?
 
Mpaka anakuwa chizi tayari ni laana unataka impate laana ipi tena?
Laani kutoka kwa nani ?

Kwahio mtu kuzaliwa Chizi nani kamlaani ?

Mtu aki-abuse drugs nani kamlaani ?, Unajilaani mwenyewe kwa either kwa your deeds au second guessing yourself
 
Hakuna mahali pameandikwa usipomuhudumia mzazi wako utalaaniwa .

Waafrika tumeendekeza imani potofu ndio maana hatuwezi kujitegemea.

Huyo mzazi kipindi chake alikua wapi asitafute hela na mali tena kipindi hiko ilikua nafuu kujipatia mali tofaut na sasa , ambapo mali hizo angerithisha wanae leo wamtunze.

Utegemezi umeanza mbalii kwenye mizizi ya koo zetu tuachane na hili swala.

Laana zipo ila haziwez mfikia mtu wa namna hio
 
Back
Top Bottom