Mtu aliyepanda miti. Umewahi kusoma hadithi hii?

Mtu aliyepanda miti. Umewahi kusoma hadithi hii?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
MTU ALIYEPANDA MITI

Hii hadithi imehamasisha mamilioni ya watu duniani kupanda miti na kutunza mazingira. Unafaa sana wakati huu tunaokabili tatizo la uharibifu wa mazingira. Umewahi kuisoma? Ulijifunza nini?

1668488178131.png




Muandishi: Jean Giono 1953.

Mtafsiri: Pictus Publishers ltd

Email: pictuspublishers@gmail.com.

©Pictus Publishers LTD 2022

Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu yoyote ya tafsiri hii inayoweza kunakiliwa, kutolewa kivuli(photocopy), kuhamishwa, kurekodiwa au kutolewa kwa namna yeyote bila ya taarifa ya awali ya kimaandishi ya mtafsiri.



Ili tabia ya binadamu iweze kuonyesha sifa za kipekee kabisa, mtu anatakiwa kuwa na bahati ya kumchunguza mtu huyo kwa miaka mingi. Kama matendo yake yamethibitika bila ya shaka yoyote kuwa hayana ujivuni, ni kwaajili ya maslahi ya wote, yametendeka bila ya wazo lolote la kulipwa na yameacha alama inayoonekana duniani, basi hapo kunakuwa hakuna shaka tena.

Kama miaka arobaini iliyopita, nilifanya safari ndefu kwa miguu kupita milima ambayo haikujulikana sana na watalii, kwenye miteremko ya milima Alps huko Provence. Wakati wa matembezi hayo, kwenye eneo hilo lililohamwa na lililokuwa kama jangwa—lisilo na rangi wala lisilozaa chochote. Hakuna kilichoota kwenye eneo lile zaidi ya urujuani mwitu.

Nilikuwa nakatisha katika eneo lake pana zaidi, na baada ya kutembea kwa takribani siku tatu, nikajikuta kwenye eneo lenye ukiwa usiolezeka. Niliweka kambi kwenye magofu ya kijiji kilichotelekezwa, nilikuwa nimeishiwa maji tokea jana yake na ilinilazimu kuyatafuta. Kwenye majengo hayo yaliyosongamana, japo yalikuwa magofu kama mzinga wa nyigu uliohamwa, lakini yalionyesha kuwa kuna mahali kulikuwa na chemichemi au kisima. Ni kweli kulikuwa na kisima, lakini kilikuwa kimekauka. Nyumba tano au sita, zilizokuwa hazina mapaa, yameng’olewa na upepo na mvua, kanisa dogo na mnara wake uliokuwa ukiporomoka vilisimama kama tu nyumba na makanisa ya vijiji vyenye watu, lakini hapa uhai wote ulikuwa umetoweka.

Ilikuwa ni siku nzuri ya mwezi wa sita, jua liliwaka vizuri, lakini kwenye eneo hili la wazi, juu kabisa milimani, upepo mkali usiovumilika ulivuma. Uliunguruma kwenye mizoga ya nyumba kama simba aliyechokozwa wakati wa kula. Ilinibidi kuhamisha kambi yangu.

Nilikuwa sijapata maji hata baada ya kutembea kwa muda wa saa tano, na hakukuwa na kitu chochote cha kunipa matumaini kuwa nitayapata. Pande zote kulikuwa na ukame uleule, na majani yaleyale magumu. Kwa mbali niliona kitu kama nguzo nyeusi na nikafikiri itakuwa ni mti. Nikaanza kuuendea. Alikuwa ni mchungaji. Kondoo thelathini walikuwa wamelala kwenye ardhi kame wamemzunguka.

Alinipatia maji kutoka kwenye kibuyu chake, baadaye kidogo akanichukua mpaka kwenye kibanda chake kilichokuwa kwenye sehemu ambayo bonde la mlima linakutanana tambarare. Maji yake aliyapata kutoka kwenye kisima kimoja kirefu cha asili. Juu ya kisima hicho alikuwa ametengeneza winchi la kienyeji kwaajili ya kuvutia maji. Mtu yule hakuwa muongeaji, na hii ni kawaida ya wale wanaoishi peke yao, lakini kwa kumuangalia, mtu angetambua kuwa alikuwa ni anayejiamini. Jambo hilo halikutegemewa kwenye nchi hii isiyozaa kitu. Makazi yake hayakuwa kibanda bali nyumba halisi iliyojengwa kwa mawe, na ilikuwa ushuhuda wa jinsi alivyofanya bidii kuyabadilisha magofu aliyoyakuta hapo. Paa lake lilikuwa ni imara. Sauti ya upepo kwenye vigae vyake ilikuwa kama sauti ya bahari ufukweni.

Makazi yale yalikuwa yamepangiliwa vyema sana, vyombo vilikuwa visafi, sakafu ilikuwa imefagiliwa, bunduki yake imepakwa mafuta, na supu ilikuwa ikichemka motoni. Na niliona kuwa alikuwa amekata ndevu zake vyema. Nguo zake zilikuwa nadhifu, hata alizoshona viraka usingeweza gundua kama zina viraka. Alinikaribisha supu na nikanywa pamoja naye, na baadaye nilipompatia tumbaku, aliniambia kuwa havuti. Mbwa wake, kama yeye tu, alikuwa mkimya lakini mwenye kujiamini.

Ilikuwa imeshaeleweka tokea mwanzo kuwa nitalala hapo usiku huo, kijiji cha karibu kilikuwa zaidi ya umbali wa siku moja na nusu. Na hata hivyo, nilikuwa navielewa vyema vijiji vya eneo lile. Vilikuwa vijiji kama vitano vilivyotawanyika huku na kule kwenye miteremko ya milima ile. Katikati ya mialoni myeupe, mwishoni kabisa mwa barabara ya mikokoteni. Vilikaliwa na wachoma mkaa, na maisha yao yalikuwa mabaya sana. Familia zilisongamana kwenye mazingira ambayo yalikuwa magumu sana, si wakati wa majira ya joto wala wakati wa majira ya baridi, wakishindwa kuepukana na migogoro isiyoisha. Huku tamaa ya watu kukimbia maisha hayo ikikua kila siku. Wanaume walichukua mikokoteni yao ya mkaa, walipeleka mjini na kurejea. Hata mtu mstaarabu vipi aliharibikiwa kutokana na ugumu wa maisha usiokoma. Wanawake walivumilia kimyakimya. Kulikuwa na uadui kwenye kila kitu, juu ya bei ya mkaa na juu ya mahali pa kuketi kanisani. Na zaidi ya yote upepo, upepo usiokoma uliotibua akili ulivuma. Kulikuwa na visa vingi vya watu kujiua na wengi kupatwa na ukichaa ambao mara nyingi ulipelekea mauaji

Mchungaji yule alienda kuleta mfuko mdogo na kumwaga rundo la mbegu mezani. Akaanza kuchambua mbovu na nzuri. Mimi niliendelea kuvuta kiko changu. Nilijitolea kumsaidia lakini aliniambia hiyo ni kazi yake. Na kwa kweli, baada ya kuona umakini aliokuwa nao alipokuwa akichambua, sikusisitiza zaidi. Hayo ndiyo yalikuwa maongezi yetu yote. Alipokuwa amepata rundo la kutosha la mbegu nzuri, alizihesabu kwenye mafungu ya kumikumi huku akiondoa zilizo ndogo au zilizokuwa zimepasuka hata kama ni kidogo. Sasa alikuwa akizichunguza kwa makini zaidi. Alipomaliza kuchagua mbegu miamoja zisizo na kasoro aliacha kazi na kwenda kulala.

Kuna amani fulani ilikuja kwa kuwa na huyu mtu. Siku iliyofuata niliuliza kama ninaweza kupumzika pale kwa siku moja. Alikubali kama alitegemea hilo au hakuna kitu cha kumshtua. Hakukuwa na ulazima wa kupumzika lakini nilitaka kumjua hata zaidi. Alifungua zizi na kuongoza kondoo wake kwenye malisho. Kabla ya kuondoka, aliloweka mfuko wake wa mbegu alizochagua kwenye ndoo ya maji.

.............
 
Back
Top Bottom