Uchaguzi 2020 Mtu ambaye Wanadamu hawakutaka aishi, lakini leo hii Mtu huyu anakwenda kuwa Mgombea wa Urais. Jambo hili lina maana gani?

Kwanza kabisa Lisu ni Mpango kamili wa Mungu.
Hili halina Ubishi. Mpaka sasa kila Mtu anamtukuza Mungu kwa sababu ya Lisu.

LISU na Nyalandu ndio wagombea wakweli wanaostahili kuwaongoza binadamu .

Hata hivyo Lisu amemzidi kidogo Nyarandu kwa kuwa panaonekana wazi Mungu ana Makusudi Fulani na Lisu.


Tuseme Ukweli kabisa pamoja na kuwa wazalendo kwa nchi yetu na kujenga ufalme wa Mungu katika nchi yetu.
Nchi yetu imegeuka kuwa nchi ya watu wasioweza kusema Ukweli.
Vitabu vya dini vinatueleza kuwa Ukweli ndio utakaotuweka Huru. Hivyo kwenye watu waongo hakuna Uhuru.

LISU NI MKWELI KULIKO WAGOMBEA WA VYAMA VYOTE WATANZANIA TULIONE HILO.
Lisu hajawahi kuwa kinyume na kauli zake katika kupigania Haki,Uhuru,Usawa,Katiba Bora,Utawala Bora na unaofuata sheria na Katiba tuliojiwekea.
LISU hajawahi kusema jambo halafu akatenda Tofauti.
Lisu akisema hii ni Nyeusi basi ni Nyeusi kweli hata ufanyeje hawezi kubadili kauli yake.

Mzalendo wa kweli ni yule anayeipigania nchi yake katika shida ,dhiki na raha .Lisu angekuwa mtu Mwingine siasa ingekua basi mana hakuna mtu wa nia mbili anayeweza kusimama kati ya Uvuli wa Mauti na kutetea kile anachoamini.
Wapo waliowasaliti wapiga kura wao kwa sababu tu ya kuona kuwa Wanaweza wakakosa Ubunge au wakashinda halafu wasitangazwe. Hao waliamua kusaliti wapiga kura wakajiunga na wale wenye nguvu ya Uteuzi.

Kuwa Mwanaharakati na mwanasiasa wa aina ya Lisu sio jambo Dogo na la mchezo. Kuna watu wanajiita wanaharakati lakini wamesimama upande wenye nguvu. Yesu hakusimama upande wa Watawala bali upande wa kundi dogo la watu dhaifu na maskini wasio hata na Chakula zaidi ya kutegemea miujiza ya mikate na samaki ili wale waishi. Lakini Leo hii Yesu ndiye Masihi Mtawala wa Haki na Mfalme juu ya Wafalme wote yaani Juu ya marais wote wa Dunia nzima na sasa anasimama katika kuujenga Ufalme usio na hila ,ufalme wa Mungu duniani.

HASARA KUBWA ALIYONAYO LISU:-

Kuongozwa na Mwenyekiti Muongo na asiye na nia njema zaidi ya manufaa binafsi ya kiuongozi.
Mwenyekiti mwenye hulka kama wenyeviti wenzake wa Vyama vyote nchini.

Uongo na kauli zisizo na nia njema za wenyeviti wa Vyama vyote:-

(1) Nimejiuzulu uenyekiti wa Chama lakini kesho anasema Mimi ndio mwenyekiti halali na vurugu juu.

Leo anasema kuwa CCM ni intarahamwe lakini kesho CCM ni chama safi nakiunga mkono.

(2) Chama changu ni cha kijamaa na kizalendo , chenye kufuata misingi ya haki na usawa bila kujali ukabila lakini akipanda jukwaani wale wa kabila lile ndio waliopendelewa na kupewa Maendeleo hivyo wasipewe tena maendeleo wasubiri (utafikiri hawalipi kodi zao) .


(3) Hiki ni Chama cha Kidemokrsia; Kesho , hiki chama Mimi peke yangu ndio nimekijenga siwezi kuruhusu uchaguzi huru wa kumpata Mwenyekiti zaidi yangu mana wengine wote ni wasaliti.

Walitaka kuniua wamenipiga wakanivunja mguu; kumbe ameanguka kwa ulevi wake wa gongo aina ya Konyagi.
Tunataka Katiba mpya Yenye mgombea huru na Uhuru wa mawazo ,Kesho unasikia kamfukuza mtu aliyetoa maoni yake kwenye chama ili akose Ubunge. Ingekuaje kama unajali mgombea Huru.

Tupo Karantini kwa sababu ya Korona ,kesho anashinda kwenye baa na kukesha mpaka usiku wa manane na akina chuchu. Uongo mtupu.

Na uongo mwingine mwingi.

(4 ) Maendeleo hayana Vyama lakini wakiamka Kesho Hamtapata Maendeleo kwa sababu hamkunichagua na hamkumchagua wa Chama Change.

Waliobomolewa pale wote hawatalipwa. Baadae wale wasilipwe mana hawakunichagua na hawa walipwe mana wamenichagua. Kauli mbili !!

Huyu ni jipu namtumbua kwa sababu amefanya ufisadi. Kesho huyu namteua mana ni mtu safi kabisa. Utafikiri watanzania wasafi wameisha.

Mkinichagua nitajali maslahi yenu kesho maslahi yenu sio kipao mbele changu.

Msema kweli ni Mpenzi wa Mungu kesho matokeo ya kura ya kweli yanageuzwa kuwa ya uongo mana Mimi ndio nakupa Mishahara wewe mkurugenzi ( badala ya kusema walipa kodi waliomchagua huyo watendewe haki mana ndio wanaokulipa Mshahara ).

Uchaguzi utakua wa huru na haki lakini kesho itategea nimeamkaje kesho.

Na kauli nyingine nyingi zisizo na Ukweli wa kutoka Rohoni kama Mungu anavyoelekeza kuwa Ukweli utatuweka huru.

####(5) Lakini kuna Mgombea alisema wapinzani wakiingia ikulu tutaingia Msituni Leo anasema nagombea kupitia Upinzani.

Ukweli utatuweka huru.

Ili tuwekwe huru jibu ni kumtizama Mgombea mkweli asiye na kauli au ndimi mbili.

Tumuombe Mungu asimamie uchaguzi wa Mwaka huu ili tupate kiuongozi bora na msema kweli bila kujali maumivu ya kusimama katika kweli na kuupigania Ukweli hata kama unaumiza chama chake na marafiki zake.


Siwezi kutoa Mawaidha ya kumsifu Mungu bila kumlaani Shetani.

Kuna Mwenyekiti Mmoja Mlevi ,mzinzi,mwizi mkabila, mla ruzuku ya chama,mpinga kila kitu na kuwalazimisha wabunge wa chama chake kuwa kama maroboti wasio na Demokrasia ya kusifia wanapoona kuna jema la chama tawala.
Mwenyekiti huyo ameshukiwa kuwa yeye na genge lake amepanga njama mbaya dhidi ya Lisu ili asingizie kuwa ni serikali.
Huyo sio mwingine Bali ni yule yule mwenyekiti wa kudumu wa Chadema. Akakanushe mana Mwanaharakati huru Musiba ameweka hadharani hizo njama ovu za huyo mwovu na mlaghai.
Kama ni kweli Mbowe shindwa na ulegee.
 
Tusubiri tuyaone maajabu ya Mwenyezi Mungu. Mungu ndiye mpangaji wa kila jambo
 
Umechambua vema sana
 
Ukweli ni kwamba,bila kujali matokeo yatakuwaje,mpaka hapa wahusika wamepata funzo kubwa sana.
Ukweli ni kuwa hadi hivi sasa Tundu Lissu ndiye mshindi.........

Huko kwenye uchaguzi mkuu, hata kama, Tume ya uchaguzi, watachakachua matokeo, lakini ifahamike tu ya kwamba Tundu Lissu ndiye chaguo la Umma wa watanzania
 
Apangalo Mola huwa

Tusubiri Oktoba 2020
 
Mungu anataka awe rais
 
Me namkubali sana Lissu ila Wewe jamaa unapenda sana kujifariji na bahati mbaya Chadema uchaguzi huu haitapata hata kura laki 5 achilia mbali kiti cha ubunge
 
Sipati picha kwa mara ya kwanza CCM wanakuwa wapinzani nchi hii. Aisee tutaona mengi mnoo.
Wengi wataugua ukichaa rasmi. Wanaotumia vidonge vya kutuliza ukichaa sijui watakuwa na hali gani.
Ila ni ndugu zetu, hatuwezi kuwatupa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…