Mtu anabebaje tuzo kwa kupiga ma playback?

Mtu anabebaje tuzo kwa kupiga ma playback?

Natabiri hoja hii kuibua malumbano makali.
Badala ya watu kujadili kilicholetwa hapa mbele yetu.
 
Labda ktk washiriki wote hakuna anayepiga live, kwa hiyo sio ajabu huyo anayepiga playback kushinda tuzo.
 
Kwan kuna "Playback award" au Live Performance award?
 
wakuu hivi inakuaje msanii anabeba tuzo kibao kwa kutegemea mziki wa playback tu?

kwa ninavyoona mimi sisi kama Tz bado hatujafikia level ya kupiga mziki wa live hasa kwenye majukwaa ya wazi, hatujawa na uwezo wa kumiliki vyombo hivyo bado
 
wakuu hivi inakuaje msanii anabeba tuzo kibao kwa kutegemea mziki wa playback tu?

Hapa ulikua unamaanisha msanii gani!?

Kama ulikua unamaanisha Diamond, mbona huyo mkali wa bongo fleva ni mkali wa live show pengine kuliko hata huyo msanii wako!

Kuthibitisha hilo embu tafuta ile show ya Diamonds are forever ujionee kijana anavyokupigia live show ya kiwango cha juu!

Au nenda youtube kaangalie show za coke studio uone kijana anavyokupigia live show za high class na wasanii wa kimataifa.

Mojawapo hii hapa

Mdogo Mdogo, Diamond & Yemi Alade, Coke Studio Af…: http://youtu.be/jxSfgsF2LPI
 
Naomba unitajie tuzo zinazo tolewa kwa kuzingatia muziki wa live!

Hakuna tunzo inayo tolewa kwa kuangalia muziki unapigwaje!

Anataka kujua kama bendi itawapa tuzo ila bila kumsema kiaina Chibu siku yake haikai vizuri.
 
Lukelo siku moja funguka basi tatizo haswa ni nini kumsaka Chibu labda tutakupa ushauri mzuri nawe utafurahia...

Nasubiri kesho utauliza nini...ila kamanataka kupaa kwa mnachofanya kuna njia nyingi hata kama ukigeza inaruhusiwa na kuomba ushauri poa pia.

So usisikie aibu...bali usitake mshusha unayemtamania mafanikio yake.
 
Lol yaani mie ndio nimeingia humu now, swali zuri umemuuliza.
huyu si unajua huwa anarukaruka tu kama maharage huwa hajibu....nnachompendea sakafu kila siku lazma ampe promo dai humu yani anamfanya kila siku tumuongelee mi napenda kwa kweli
 
kwa ninavyoona mimi sisi kama Tz bado hatujafikia level ya kupiga mziki wa live hasa kwenye majukwaa ya wazi, hatujawa na uwezo wa kumiliki vyombo hivyo bado
Asikuambie mtu Paula... playback haiepukiki na wala haitakuja kufutika unless aina ya utengenezaji wa muziki ibadilike. Na hii si kwa Tanzania tu bali hata kwenye mataifa mengine; na hata huko US bado mpaka kesho wapo watu kibao tu na matamasha kibao tu ambayo watu wanatumia playback kwahiyo ni kichekesho cha mwaka msanii yeyote ambae utengenezaji wa muziki wake unaanzia studio halafau akasema hatatumia tena playback! Na moja ya mijadala ya kimuziki duniani ambayo bado hadi leo haijapata consensus ni suala la which's which kati ya Playback na Live Performance! Kuna watu kibao ambao wanaamini aina fulani ya muziki ukifanya live performance unashindwa kuipata taste yake... na hii ni ile aina ya muziki ambayo huanzia studio na kwenda kwa mlaji!
 
huyu si unajua huwa anarukaruka tu kama maharage huwa hajibu....nnachompendea sakafu kila siku lazma ampe promo dai humu yani anamfanya kila siku tumuongelee mi napenda kwa kweli

He is obsessed with Diamond
 
Back
Top Bottom