GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Hata kama amekasirishwa, kutukana kutamsaidia?
Nimo kwenye basi naelekea mkoa fulani. Njiani, mama mmoja kapitilizwa na konda kituo alichopaswa kushukia.
Kutokana na kukerwa na hiyo hali, aliposhuka, hakulalama tu, bali pia alisindikiza manung'uniko yake na tusi la nguoni. Alitukana kwa kutaja sehemu za siri za mwanamke.
Kwa kuwa aliyefanya hiivyo ni mwanamke, atakuwa amemtukana konda ambaye ni mwanaume au kajitukana mwenyewe?
1. Kama ni uke, yeye naye anao! Siyo kwamba amejitukana?
2. Hakuna kitu cha ajabu kwa mwanamke kuwa na uke. Kila mwanamke wa kawaida yuko nao. Kulikoni watu wanapokasirika hutumia huo msamiati kama fimbo ya kuwaadhibu waliowakasirisha?
3. Mwanaume anapomtukana mtu mwingine kwa kumtukania sehemu za siri za mama yake, naye si kwamba kajitukana? Kwani yeye mama yake hana?
Huwa nawaona wanaowatukana wenzao kwa kuwatukania sehemu za siri za mama zao kama wana tatizo la kiakili. Huo ndiyo mtazamo wangu.