Mtu anapomtukana mwenzake anafaidi nini?

Hujiulizi kwanini NYOKA anatema mate ovyo au kugonga sehem mbalimbali..

Na akifanya hivyo ana relax kwa muda..?
Akishatema mate na kurelax na ghafla akatokea adui, bado atakuwa na uwezo wa kujitetea? Hatakuwa ameshafilisika silaha (sumu) kutokana na matumizi mabaya?

Kadhalika, mtu anayechokoneka kirahisi hisia zake, Kisaikolojia, anahesabiwa kuwa ni mdhaifu sana.

Ustaarabu unapimwa na kiwango cha mtu kuweza kutawala hisia zake.

Ikiwa hawezi, huyo hufananishwa na wanyama wa kawaida.
 
Inategemea.. kuna Nyoka aina ya BLACK MAMBA yeye ni yupo tofauti kabisa..

Anaweza kugonga hata mara 70 na bado akawa vile vile...... na akizaliwa kitoto kidg sumu yake ni ile ile kama ya mkubwa...
 
Suala la kutukana ni malezi na makuzi ya mtu. Infact kuna watu wao kutamka matusi kwao ni kawaida tu hata katika maongezi ya kawaida. Mimi binafsi huwa siwezi kabisa kutamka maneno ya matusi hata iweje, na hua namshangaa mtu anaetamka matusi hasa mwanamke.
 
Huku kwetu starehe ya walevi wakishalewa ni kuporomosha matusi non stop [emoji23]
 
Hakuna faida yoyote kumtukana mtu zaidi ya kujiongezea uadui siku Hadi siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…