Mtu anaye/aliyevunja Katiba,dawa yake ni kuondoka hata kwa kufanyiwa alichofanya

Joined
May 30, 2020
Posts
67
Reaction score
108
Dear Members, Heri ya Mwaka Mpya 2022,

Leo nikiwa nafanya ibada ya asubuhi nikiombea Nchi yetu pamoja na viongozi wake, Neno la Bwana likanijia kwa sauti ya upole likisema ..ewe Mwanadamu, andika hivi " Kwa kuwa mshahara wa Dhambi ni MAUTI na kwa kuwa kila KOSA lazima liadhibiwe na kwa kuzingatia Mungu ni HAKI na hana upendeleo juu wa wanaoivunja sheria ya Bwana na kwa kuzingatia kuwa imeandikwa MWENYE HAKI WANGU ataishi kwa IMANI, hivyo basi saa imefika ya walioihalifu sheria ya Bwana kuvuna matunda ya mikono yao mbele ya uso wa waliokuwa wanawashangilia na kuwaona ni mwema kumbe wamevaa ngozi ya kondoo japo ndani ni Mbwa Mwitu anayerarua wasiokuwa na HATIA" Asema Bwana wa majeshi.

Sasa kwa kuzingatia kuwa kuanzia karne ya 4 (320 A.D) hadi mwishoni mwa karne ya 11 (1000 A.D) wakati dola ya RUMI (Roman Empire)ilipoanza kuitawala dunia kaba ya kuanguka rasmi mwishoni mwa karne ya 15, ilikuwa viongozi wa Kanisa na viongozi siasa ni wamoja na kauli zao ndio za mwisho. Jamii iliamini kuwa uongozi umetoka kwa Mungu na wote walio kwenye mamlaka wametokana na Mungu (DARK AGE). Kuanzia karne ya 16 wakati Ulaya mashariki inapitia kipindi cha ENLIGHTMENT AGE watu walianza kufanya logical reasoning na vitabu kadhaa viliandikwa na wasomi kama akina John LOCKE kuhusu SOCIAL CONTRACT na SEPARATION OF POWERS by DICEY/MONTESQUIE na wenzake. wakati wa mapinduzi ya Viwanda, jamii ilianza kuendeshwa kwa logical na haki za binadamu zilianza kuzingatiwa hasa baada ya Mkataba wa Magna Carter wa 1225 huko ENGLAND. Kwa hiyo, kuanzia karne ya 17 kuja ya 18, Siasa na Dini vilitenganishwa na ndipo KATIBA ikawa mbadala wa BIBLIA katika kuwaongoza watu wa wote kwa kuzingatia kuwa wameumbwa kwa sura na Mfano wa MUNGU. Jamii za Kiafrika zilianza kuwaondoa Wakoloni katika nusu ya karne ya 20 hasa baada ya kuamini kuwa Wakoloni hawakutokana na Mungu bali binadamu wenye roho mbaya wanaowatendea vibaya wenzao.

Naomba kuwaalika kuangalia kwa nini Mataifa/Jamii zilianza kuendeshwa kwa KATIBA? Hii ni kwa ajili ya kuweka MIPAKA ya OFISI/NAFASI na majukumu ya kila ofisi ili kuepukana na migongano isiyokuwa na ulazima. Tanzania nayo kama Jamhuri/Nchi zingine za Jumuiya ya madola/commonwealth inaendeshwa kwa KATIBA kuanzia 1961 na hadi sasa tunatumia KATIBA ya mwaka 1977.

Mwishoni mwa mwaka 2021 na mwanzoni mwa 2022 yametokea malumbano ya HOJA kwenye uwanda wa siasa za Tanzania baada ya Mzee mmoja akiongea na watu wa kabila lake kusema kuwa ipo siku
NCHI hii ITAPIGWA Mnada kwa sababu ya MADENI ya Nje yanayofikia Trilioni 70" Mzee huyo amejibiwa kuanzia kila kona ya Nchi kutokana na HOFU ya watu kupigwa mnada pamoja na wapenzi/wazazi wao au na mali zao; hata nami nilipatwa na woga kuwa ipo siku naweza kujikuta kwenye mnada wa Benki ya Dunia; ndio maana nikaamua kuwaalika kwenye MIPAKA YA KATIBA YETU.

Kwa kuzingatia HOJA yenyewe bila kumpuuza au kumkosea heshima MTOA hoja, nashawishika kuamini kwamba wengi wetu bado ni wageni wa issue ya SEPARATION OF POWERS na Checks & Balances= Kati ya mwaka 2016 hadi 2020 BUNGE la Nchi ya USA lilijaribu mara 2 kumwondoa Madarakani Donald Trump bila mafanikio kutokana na checks and balances ya Bunge kwa Mhimili wa Executive. Kwa hiyo ni raha kama kila MTU atacheza ndani ya MIPAKA yake bila kuguza PUA ya mwenzake= Kila mhimili ubane haswa nafasi yake kama ilivyo kwenye Katiba ila sio fitna na chuki za hovyo hovyo.

Ibara ya 3 ya Katiba yetu ya mwaka 1977 inatangaza kuwa Nchi hii ni ya Kidemokrasia, inayofuata mfumo wa vyama vingi na haina dini na ibara ya 4 inaelezea dhana ya MIHIMILI 3 ya DOLA,Bunge, Mahakama na SERIKALI ambavyo vyote hufanya KAZI kwa ajili ya Mwananchi sawa na ibara ya 8(b).

Bunge limeanzishwa kwa ibara ya 62 hadi 103 na miongoni mwa majukumu yake ni KUPITISHA BAJETI YA SERIKALI sawa na ibara ya 101 hadi 103. Mwaka wa fedha 2021/2022 SERIKALI iliomba kuidhinishiwa na BUNGE Bajeti ya Trilioni 31 na ilipitishwa na miongoni mwa vyanzo vya kupata hayo mapato ni pamoja na KODI,TOZO,USHURU, MISAADA,MIKOPO nk


Kwa mantiki hiyo Bunge limeipatia kibali cha KUKOPA na kwa mujibu wa sheria za Tanzania, Wizara Waziri/ wa FEDHA ndiye MTU pekee anayeidhinisha mikopo/misaada na misamaha ya kodi. Kwa hiyo HOJA ni kwamba serikali imefanya hivyo kwa idhini ya BUNGE la Julai 2021 na waziri husika alitaja vyanzo vya mapato ni pamoja na mikopo. (Rejea Hansard za Tarehe 16 hadi 21 June 2021) Mapato ya Ndani ya Tanzania kwa mwaka ni takribani trilioni 16 hadi 20, kwa hiyo bajeti ya trilioni 31 inakuwa na nakisi (deficit) ya Trilioni 11, ambayo itapatikana kwa mikopo na misaada ya NJE.

Kwa hiyo basi, BUNGE lilitimiza wajibu wake KIKATIBA kupitisha Bajeti ya Trilioni 31 na serikali inatimiza wajibu wake kutafuta vyanzo vya mapato ikiwepo MIKOPO ili kuifikia bjaeti iliyopitishwa na BUNGE.


UGOMVI unatoka wapi? Ni kwa sababu watu hatuelewi maana ya separation of Powers na kuiheshimu KATIBA.

MTU ambaye amewapokewa watu waliofoji nakala za serikali, wakajitangazia kuwa ni wawakilishi wa chama ambacho kimewakataa, na akawaapisha bila uhalali wa KISHERIA /KIKATIBA au KISIASA ni mhalifu kama wahalifu wengine na anatakiwa kuadhibiwa na kuondolewa ama kikatiba au kuikiukat Katiba kama yeye alivyofanya. Kwa mujibu wa Katiba yetu ibara ya 67(1)(b) kwamba MTU hawezi kuwa Mbunge isipokuwa kwa kupendekezwa na chama cha siasa, sasa kama katiba inakanyagwa na namna hii, kwa nini tusiikanyage kwa kumwajibisha huyu mtu anayeingilia utendaji wa MHIMILI mwingine kinyume cha sheria?

Ibara ya 78(3)(4) inaelekeza namna ya kuwapata wawakilishi wanawake kupitia vyama vya siasa, sasa mtu ambaye haheshimu Katiba, anawezaje kulindwa na kitu ambacho yeye anaivunja?

Waingereza wana msemo kwamba, "You cannot eat your cake and have it", kama umeamua kuivunja katiba yetu, inawezaje kukulinda wewe? Kwa hiyo basi, masharti ya Katiba ibara ya 71(f)(g) yanaweza kutumika kukamilisha kwa mtu aliyekula KEKI yake huku anataka kuwa nayo.

Kwa ibar aya 98 niJUKUMU la serikali kukopa na Mikopo yote inalipwa na serikali sio Bunge.

Nasimama na Mhimili wa SERIKALI ili kuweza kuitekeleza Bajeti ya serikali ya Trilioni 31 iliyopitishwa na BUNGE la Julai 2021, kwamba mapato ya Ndani ni Trilioni 17hadi 20 na MIKOPO/MISAADA ni Trilioni 11; Hoja ingekuwa nzuri kama SERIKALI imefanya kinyume na kile ambacho BUNGEm(Wananchi) limepitisha,

so long they are within their lines, let players kick the ball to win the match against poverty, diseases and ignorance"

"GOD BLESS TANZANIA, BLESS OUR GOVERNMRNT AND THE HEAD OF EXECUTIVE"
 
Hata kama una hoja sio kwa mirangi hiyo. Inakuwa kama mtu anayejifunza Microsoft word eneo la format!
 
Wengine tuna bad eye sight tumeshindwa kusoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…