Mtu anayetoa milion 10 kununua bajaji Ili apewe 20k Kwa siku ni kufanya biashara kichaa

Mtu anayetoa milion 10 kununua bajaji Ili apewe 20k Kwa siku ni kufanya biashara kichaa

Ni biashara ya kifala kweli, ila biashara nyingi faida yake ni ndogo pia cha msingi ni mzunguko wa fedha usiende mbali na wewe.
unaijua biashara ya hardware hii ni manyoko usipouza stock kubwa kwa mwezi mmoja tu
Mkuu hiyo Hardware imekaaje coz nataka niifanye
 
Sasa boss unakuwaje dereva tena? Dhana ya kwamba ukijiajiri unakuwa huru, hapo inadhihirikaje?
Uhuru wa kujiajiri ni muda, sijui ww ulikuwa unafikiria uhuru gani. Uhuru wa muda wa kufanya chochote muda wowote. Ukiwa mmliki wa bajaj kwamba ndo hutakiwi kuwa dereva? Asee we jamaa kama una mentality hii, utafeli sana kwenye business. Endelea na iyo ajira yako tu.
 
Yaani Kuna watu akili kama zimepungua kichwani hivi unanunua bajaji milion 10 halafu unampa mtu mmoja awe anapiga deiwaka anakuletea 20k Kila siku na risk za kutosha hii ni akili Gani yaani hela za mashamba ya urithi nyumbani kwenu unatarajia hii biashara kichaa ikunufaishe aisee kweli washamba mnaotoka kijijini na pesa za urithi wa mashamba mtaendelea kukumbatia umasikini milele?
Daaah aisee 😅
 
Biashara kichaa hiyo
We jamaa hii ndo hoja yako pekee tu "biashara kichaa". Alafu umeelezea/kugusa upande mmoja tu wa mmiliki kumpa mtu aendeshe amletee hesabu ya 20k (huyu ndiye anafanya biashara kichaa), hujagusa upande wa mmiliki ambaye ataamua kuendesha/kukomaa mwenyewe (huyu hafanyi biashara kichaa kama unavyowaza wewe). Alafu usikariri mzee sio kila bajaji hesabu ni 20k, kuna bajaj za NMB hesabu ni 15k per day, na ni mkataba 2 yrs.

Bajaj ukizingatia service kwa wakati na vitu vidogo vidogo na ukaamua kukomaa mwenyewe faida ya unachokifanya utaiona. Ila tofauti na hapo ndo nitakubaliana na wewe kuwa ni biashara kichaa.

NB; hamnaga biashara rahisi na kila biashara ina ukichaa wake, ni namna utakavyo changa karata zako kwenye iyo biashara unayoifanya.
 
Yaani Kuna watu akili kama zimepungua kichwani hivi unanunua bajaji milion 10 halafu unampa mtu mmoja awe anapiga deiwaka anakuletea 20k Kila siku na risk za kutosha hii ni akili Gani yaani hela za mashamba ya urithi nyumbani kwenu unatarajia hii biashara kichaa ikunufaishe aisee kweli washamba mnaotoka kijijini na pesa za urithi wa mashamba mtaendelea kukumbatia umasikini milele?
Ww ndio huna akili kabisa unataka afanye nini kama ww huna akili vizuri usilazimishe na wenzako wabishi kama ww
 
Asee we jamaa kama una mentality hii, utafeli sana kwenye business. Endelea na iyo ajira yako tu.
Hao waliopo kwenye business wamefaulu? Mbona sasa wanalalamika kwenye uzi huu huu?
 
Kuna watu akili kama zimepungua kichwani hivi unanunua bajaji milion 10 halafu unampa mtu mmoja awe anapiga deiwaka anakuletea 20k Kila siku na risk za kutosha hii ni akili Gani yaani hela za mashamba ya urithi nyumbani kwenu unatarajia hii biashara kichaa ikunufaishe aisee kweli washamba mnaotoka kijijini na pesa za urithi wa mashamba mtaendelea kukumbatia umasikini milele?
Kuna dogo mmoja wa kiarabu pale mwananchi anazi kumi Sasa sijui kati yako na yeye nani mjanja
 
Tupe hesabu zako basi zinazosibitisha uchizi wake??
20,000x365days= 7,300,000 hiyo ni kwa mwaka mmoja.
Hahahahah km biashara ingerikua ivyo kila mtu angerikua tajiri akunaga hesabu za kijinga ivyo ktk biashara

Na km iyo million 7 inapatikana kirahisi ivyo why vijana wanazirudisha kwa matajiri why mnawakopesha watu mpaka miaka3
 
Na anaenunua bus jipya na kumkabidhi mtu ambae atamletea kiasi fulani cha pesa kwa siku imekaaje? Angalia gharama ya bus na kiasi cha pesa kwa siku!
 
Km unaweza pata milion10 ya kununua bajaji kwa nn kwa iyo milion10 usitafte IST,passo, rush ya namba C ama D ukaifanya uber na pia ukaikodisha kwenye harusi na sherehe, misiba

IST,passo / rush inaweza dumu miaka 20 ila bajaji ata uwe mtunzaji vp huwez maliza nayo miaka 7
 
Hao waliopo kwenye business wamefaulu? Mbona sasa wanalalamika kwenye uzi huu huu?
Hao waliofeli kwenye business ya bajaj walikuwa na mentality kama yako. Kwamba mimi ni boss nitafute mtu aniendeshee chombo.
Kuna teacher mmoja nipo nae kitaa, jamaa amechukua bajaj ya NMB akaingia road ye mwenyewe. Asubuh anaamka mapema anapiga route zake anaunganisha na chombo hadi school, jion akitoka anapiga tena route zake kadhaa anaunganisha home. Walimu wenzake wakat ameanza kwenda na bajaj school walimuona mwehu kwann asingenunua gari, ila sahv wanamuelewa anachofanya. Jamaa halii shida kama walimu wengine. Jamaa ni mwalimu wa primary.
Jamaa ni mteja wangu wa service na anapiga service kwa wakati, chombo yake ni no D zile za mwanzoni ila imesimama kama no E.
 
Back
Top Bottom