Mtu anayetoa milion 10 kununua bajaji Ili apewe 20k Kwa siku ni kufanya biashara kichaa

Mtu anayetoa milion 10 kununua bajaji Ili apewe 20k Kwa siku ni kufanya biashara kichaa

N bora utafute haic kwa ml 10 kwa siku ikuletee ata 35000 kama sio 50 hata kama itapak kifuru au kibeberu uko ndan ndan
 
Onyesha hata million 1 tu kwenye account Yako 🤣🤣🤣🤣
Wanawake mna matatizo kweli?

Yaani Mimi kidume muda wa kuweka pesa kwenye akaunti za Vikoba mtandaoni natoa wapi?,niache kuweka pesa benki Kwa ajili ya familia yangu niweke kwenye akaunti ya Vikoba ili nikuonyeshe wewe!,Halafu nikikuonyesha napata faida gani?

Wanawake mna matatizo kweli!
 
Biashara ya bajaji na kuweka fedha fixed au UTT ni biashara ambazo mtu unatakiwa ufanye kama tayari una 60 yrs.
Yani kijana upate 10M halafu uisubiri kwa miaka 2 ndio urudishe pesa ni ukichaa,huku hata ukialangua mahindi Mkoa wa Songea kwenda Mwanza unaweza rudisha 10M yako ndani ya miezi 4.
Chief Songea mahindi yanakuwa tayari kuanzia mwezi wa ngapi?
 
Biashara ya pikipiki/gari inahitaji usimamizi wa karibu, vinginevyo utamtajirisha dereva.
 
"Biashara ni wewe mwenyew" mambo ya kusema wewe unakunja 4 unategemea mtu humjui hakujui et akufaidishe ww Mhh sahau, Kama unanunua bodaboda, bajaji sijui umefungua salun hakikisha unaiendesha ww mwenyew au kama ni ofisi na umeajiriwa hakikisha unatenga masaa Yako kadhaa ya kukaa kwenye ofisi Yako Kila siku bila hivo utalia Kila siku biashara mbaya...Sasa kama huyu aliyenunua Bajaj 10M eb imagine angekuwa anaendesha mwenyew mapema sana unarudisha pesa yako, faida juu na usalama wa chombo uhakika.
 
Yaani Kuna watu akili kama zimepungua kichwani hivi unanunua bajaji milion 10 halafu unampa mtu mmoja awe anapiga deiwaka anakuletea 20k Kila siku na risk za kutosha hii ni akili Gani yaani hela za mashamba ya urithi nyumbani kwenu unatarajia hii biashara kichaa ikunufaishe aisee kweli washamba mnaotoka kijijini na pesa za urithi wa mashamba mtaendelea kukumbatia umasikini milele?
Ulishatoka kwa shemeji yako? Ni aibu baba mzima karibia miaka 40 bado uko kwa shemeji!
 
Akili zenu zina shida! Ina maana huyo anayepeleka rejesho habakiwi na kitu mkononi?
Bora anaetoa pesa yake cash, akikomaa mwenyewe pesa yake ataiona.

Nawaona wajinga wale wa kuchukua bajaj za mkopo halafu kila siku upeleke 20,000 ya marejesho kwa miezi 36. Unakuta unainunua hiyo Bajaj hata mara 3.

Unamaliza kulipa deni na Bajaj imekufa.
 
Hicho kitu hata mimi nakipinga sana bora kununua guta na huwa linaleta hela nyingi na bei yake huwezi fananisha na bajaji
 
Yaani Kuna watu akili kama zimepungua kichwani hivi unanunua bajaji milion 10 halafu unampa mtu mmoja awe anapiga deiwaka anakuletea 20k Kila siku na risk za kutosha hii ni akili Gani yaani hela za mashamba ya urithi nyumbani kwenu unatarajia hii biashara kichaa ikunufaishe aisee kweli washamba mnaotoka kijijini na pesa za urithi wa mashamba mtaendelea kukumbatia umasikini milele?
Wakati mwingine inawezekana hategemei hii hela kwa matumizi ya moja kwa moja na sio kila biashara inategemea ile faida ya fedha ya wakati huo. (hatumii money one) kama tulivyozoea.
mfano mfugaji anaweza kuamua kuuza maziwa ya ng'ombe wake kwa lita moja shs 1300 wakati wengine wakauza kwa shs 2000 na unaweza usielewe lakini yeye faida yake anaipata kwenye kinyesi cha mfugo wake ikiwa ni pamoja na kuchakata gesi mbolea kwa ajili ya mbogamboga.
 
Back
Top Bottom