Mtu anayetoa milion 10 kununua bajaji Ili apewe 20k Kwa siku ni kufanya biashara kichaa

Mtu anayetoa milion 10 kununua bajaji Ili apewe 20k Kwa siku ni kufanya biashara kichaa

kinachoumiza kichwa ni kwamba biashara hii inamnufaisha dereva dogo ila kwa tajiri kwako kutoa 10m kununua bajaj mpya labda uendeshe mwenyewe. utakua na uchungu nq mali yako.nishakuta bajaj imekula gunia za mkaa kama 10. hiv ungekua mwenyewe ungefamya? au unakuta dogo anaenda gest na demu anachokifanya anampa deiwaka. deiwaka anaenda kupiga shimo huko njia mbov na yeye apate.
endeshq mwenyewe hela itarud
 
Kwa maoni yangu kumpa mnyoa kiduku(virasta) bajaji ya milion 10 kwa rejesho la 20k per day ni uongo nazani wamiliki wa bajaji wangewaiga MO FINANCE na WATU rejesho per day 25k hadi 30k inategemea na kianzio na bado kuna kianzio ndio kitaamua rejesho lako vijana wanazigombania mno

Hii biashara ina pesa kama utaamua kuingia mwenyewe barabarani pesa utaiona haswaa. Mimi pia natarajia kuingia kwenye hii biashara maana nimeshamaliza process zote na bank ya CRDB bado kukabiziwa chombo changu

Bank wana mikataba mizuri na rejesho nafuu mimi nikipata chombo natakiwa nirejeshe 17k per day na dereva ni mimi mwenyewe kwa sasa nimechukua likizo ya miezi miwili kazini nataka nijaribu upande wa bajaji na pia ninampango wa kuomba miezi miwili tena bila malipo nazani kwa miezi 4 nitapata picha halisi kati ya biashara ya bajaji na kazi ninayofanya kipi ni bora

Tusikatishane tamaa kwa kusema biashara ya bajaji hailipi changamoto zipo kwa kila biashara sema wengi tunapenda umwinyi umenunua bajaji unamkabizi kiduku (virasta) bila kujua changamoto ya biashara kwa undani hapo shida ipo
 
Yaani Kuna watu akili kama zimepungua kichwani hivi unanunua bajaji milion 10 halafu unampa mtu mmoja awe anapiga deiwaka anakuletea 20k Kila siku na risk za kutosha hii ni akili Gani yaani hela za mashamba ya urithi nyumbani kwenu unatarajia hii biashara kichaa ikunufaishe aisee kweli washamba mnaotoka kijijini na pesa za urithi wa mashamba mtaendelea kukumbatia umasikini milele?
Kichaa ni mtu anayejenga nyumba kwa milioni 80, na kuipangisha kwa 300,000 kwa mwezi au 10,000 kwa siku. Mwenye akili ni yule aliyenunua bajaji kwa mil, 8 na kupata 600,000 kwa mwezi au 20,000 kwa siku. Aliyejenga nyumba hela yake itarudi baada ya miaka 22 au miezi 264 na bajaji atarudisha baada ya mwaka mmoja na miezi miwili. Au jumla ya miezi 14.
 
Yaani Kuna watu akili kama zimepungua kichwani hivi unanunua bajaji milion 10 halafu unampa mtu mmoja awe anapiga deiwaka anakuletea 20k Kila siku na risk za kutosha hii ni akili Gani yaani hela za mashamba ya urithi nyumbani kwenu unatarajia hii biashara kichaa ikunufaishe aisee kweli washamba mnaotoka kijijini na pesa za urithi wa mashamba mtaendelea kukumbatia umasikini milele?
Hii ni biashara ambayo inafanyika wewe ukiwa kwenye shughuli zako nyingine, imagine umenunua mbili that's 40,000/- per day yaani umeachana na kusumbuliwa hela za mchicha na vitunguu nyumbani hausumbuliwi whilst kila anaendelea na shughuli zake nyingine.
Kwahiyo ukiwanazo mbili ni 1,200,000/- kwa mwezi ilhali kila mtu akiendelea na shughuli zake nyingine kama kawaida.
Nyumba ni uwekezaji permanent lakini kama umejenga nyumba ya biashara ambayo utapata kodi ya 1,200,000/- itakuwa imekugarimu uwekezaji wa kiasi gani kuanzia ununuzi wa kiwanja mpaka ujenzi?
Angalizo:Kama una mtaji wa kujengea nyumba ya biashara jenga nyumba lakini kama una mtaji mdogo unaotosha kununua bajaji basi ni bora ununue bajaji.
 
Hizo ni biashara za watu wavivu wasiotaka kuwajibika, ukiwakuta huko makazini wanavyojisifu utaskia

" Nina bajaj yangu nimempa kijana kwa week napata 140k yangu nna wasiwasi gani "

😀😀😀

Ikipita miez kadhaa unakuta kaomba likizo ya dharura ofisini ukiuliza anafatilia kesi yake na dereva wa bajaji.. kisa anamchakachua
 
Una suggest biashara gani afanye mtu mwenye mtaji wa 10M ? 😎

Maana uzi wenyewe huu umecopy na kupaste hapa from X(twitter).
 
"Biashara ni wewe mwenyew" mambo ya kusema wewe unakunja 4 unategemea mtu humjui hakujui et akufaidishe ww Mhh sahau, Kama unanunua bodaboda, bajaji sijui umefungua salun hakikisha unaiendesha ww mwenyew au kama ni ofisi na umeajiriwa hakikisha unatenga masaa Yako kadhaa ya kukaa kwenye ofisi Yako Kila siku bila hivo utalia Kila siku biashara mbaya...Sasa kama huyu aliyenunua Bajaj 10M eb imagine angekuwa anaendesha mwenyew mapema sana unarudisha pesa yako, faida juu na usalama wa chombo uhakika.
Ukiwa na bajaji 3 utaendesha vipi Mwenyewe?.
 
Yaani Kuna watu akili kama zimepungua kichwani hivi unanunua bajaji milion 10 halafu unampa mtu mmoja awe anapiga deiwaka anakuletea 20k Kila siku na risk za kutosha hii ni akili Gani yaani hela za mashamba ya urithi nyumbani kwenu unatarajia hii biashara kichaa ikunufaishe aisee kweli washamba mnaotoka kijijini na pesa za urithi wa mashamba mtaendelea kukumbatia umasikini milele?

Ila una hoja.. bodaboda ya 2m+ kwa siku 10k bajaji ya 10m kwa siku 20k..

So kwa boda inabidi asubiri
almost miezi 9 au apate mtaji wake kisha miez kadhaa ya faida..

Dah hapa ule msemo the high the risk the high the return unakuwa na ukakasi boda na bajaji risk kubwa return ndogo yaani bajaji return ya chini ya 1% kwa mwez ni ndogo sana
 
Yaani Kuna watu akili kama zimepungua kichwani hivi unanunua bajaji milion 10 halafu unampa mtu mmoja awe anapiga deiwaka anakuletea 20k Kila siku na risk za kutosha hii ni akili Gani yaani hela za mashamba ya urithi nyumbani kwenu unatarajia hii biashara kichaa ikunufaishe aisee kweli washamba mnaotoka kijijini na pesa za urithi wa mashamba mtaendelea kukumbatia umasikini milele?
Chukia hiyo mil 10 halafu tuleteee biashara isiyo na kichaaa ndani yake. Unaonekana kwenye biashara wewe ni mweupe kichwani mara 1000
 
Ungeiweka benki, angalia faida yake kwa miaka 2 na ucheki utakuwa umeingiza ngapi kwa bajaji. Ni uvumilivu tu na kuomba majanga yapite mbali. Kuliko kuweka pesa benki izungushe wewe mwenyewe.
 
Back
Top Bottom