Sasa moderators labda mtueleweshe
Payge
Active
Sasa mbona kama.hii mada ni ya kukejeli biashara za vijana waliojiajiri na wenye kufanya hii biashara?
Mleta mada mwenyewe hakuna popote ambapo anaongea kwa hoja na lugha za mtu mwenye akili anaejitambua zaidi naona MATUSI FEDHEHA NA KEJELI, mlifanya vyema kuindoa hii mada mwanzon ila nashangaa mmeirudisha tena
Hii mada imeletwa kwa lengo la kukejeli na kudharau biashara za watu ambayo imeweza kuleta positive impact kubwa kwa vijana badala ya kukaa vijiweni na kutukana kuongea ujinga na kuvuta bangi mtu unakua bize na wateja na kujipatia rizki na kipato.
Nilitegemea kungekua na mada ambayo inafundisha labda namna bora zaid ya kufanikiwa kwenye hii biashara, ila naona ni matusi dhihaka na kejeli ,
Hii mada iondolewe au iwe locked.