Its Tesha
Senior Member
- Oct 6, 2025
- 168
- 608
Ndugu Humphrey Polepole akiwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi akiwapokea askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walipofika Lilongwe, nchini Malawi kutekeleza amri ya Amiri Jeshi Mkuu.
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walipeleka msaada wa kibinadamu kwa Serikali ya Malawi – chakula na vifaa vya kujihifadhi na kujiokoa kwa wananchi wa Malawi waliokumbwa na kimbunga FREDDY.
Kimbunga FREDDY kilichosababisha mafuriko yaliyoikumba nchi ya Malawi, kilitokea 13 Machi, 2023 na kusababisha madhara mbalimbali ikiwemo majeruhi, vifo vya zaidi ya watu 400, makazi, mali, miundombinu
Msaada wa kibinadamu uliotolewa ni pamoja na fedha taslim na vifaa mbalimbali thamani ya US$1,000,000. Chakula (unga) tani 1,000. Blanketi 6,000. Mahema 50. Helicopters 2 za kijeshi. Askari 100. US$300,000
Nataka kusema kwamba, mtu ambaye ametumikia Taifa kwa kiwango hiki hastahili kutekwa na kupotezwa. Hata kama yapo makosa ambayo anadhaniwa kutenda na kuvunja sheria, akamatwe na ashtakiwe.
Mtu ambaye amewahi kuhudumu kama mwenezi wa CCM Taifa, Mbunge wa Bunge la Tanzania, Mkuu wa Wilaya, hatakiwi kutekwa na kupotezwa kwa makosa ambayo ametenda – kama yapo. Utaratibu ufuatwe, ashtakiwe.