Mtu Kama Huyu Hastahili Kutekwa, Historia ya Utumishi wa Humphrey Polepole kwa Taifa

Its Tesha

Senior Member
Joined
Oct 6, 2025
Posts
168
Reaction score
608
Ndugu Humphrey Polepole akiwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi akiwapokea askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walipofika Lilongwe, nchini Malawi kutekeleza amri ya Amiri Jeshi Mkuu.

Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walipeleka msaada wa kibinadamu kwa Serikali ya Malawi – chakula na vifaa vya kujihifadhi na kujiokoa kwa wananchi wa Malawi waliokumbwa na kimbunga FREDDY.

Kimbunga FREDDY kilichosababisha mafuriko yaliyoikumba nchi ya Malawi, kilitokea 13 Machi, 2023 na kusababisha madhara mbalimbali ikiwemo majeruhi, vifo vya zaidi ya watu 400, makazi, mali, miundombinu

Msaada wa kibinadamu uliotolewa ni pamoja na fedha taslim na vifaa mbalimbali thamani ya US$1,000,000. Chakula (unga) tani 1,000. Blanketi 6,000. Mahema 50. Helicopters 2 za kijeshi. Askari 100. US$300,000

Nataka kusema kwamba, mtu ambaye ametumikia Taifa kwa kiwango hiki hastahili kutekwa na kupotezwa. Hata kama yapo makosa ambayo anadhaniwa kutenda na kuvunja sheria, akamatwe na ashtakiwe.

Mtu ambaye amewahi kuhudumu kama mwenezi wa CCM Taifa, Mbunge wa Bunge la Tanzania, Mkuu wa Wilaya, hatakiwi kutekwa na kupotezwa kwa makosa ambayo ametenda – kama yapo. Utaratibu ufuatwe, ashtakiwe.

Kina Ben Sanane ndiyo wanastahili kutekwa?
 
Baada ya kundi la wanamtandao kuchukua nchi, ndio Tz iliporomoka na kuwa mediocre katika kila sector, kumefanyika dilution katika kila standard na maendeleo yaliyofikiwa tangu uhuru, kwa sasa kila akili inafikiria pesa tu na zinatumika kila mbinu kuzipata!

Hatuna tena viwango wala position katika kila eneo, kuanzia michezo mpaka mambo yote ya kitaalam, hata jeshi letu waliomo ndani wanajua, kwa nje raia wanaliona lina viwango sana lkn waliowahi kutumikia wanajua lilivyo. Afisa wa jeshi aliyepita TMA kabla ya kina Tamimu na Hans Pope waliiva na kuwa maafisa wanaoweza kutumika popote duniani, baada ya hapo mitaala ya mafunzo ililainishwa progressively hadi sasa. Leo hii afisa wa kibongo akikutana na wa kenya tu kwa mfano anajisikia mnyonge, tunajisifia manguvu tu sio maarifa

Kwa wenye kumbukumbu na waliosoma makala za Eugene Maganga (RIP) kabla hajafariki kwenye gazeti la Rai watakubaliana nami kwamba kile kilikua kichwa na kiwango chake kukipata jeshini miaka hii ni chini ya 10% ya maafisa. Na alikuwa Luteni tu hakufikia u-captain. Walifikia kumuita msomi asiye na degree. Vijana wa kisasa haya hawayajui.

Miaka ya 80 polisi walikuwa mpaka na uwezo wa kupata alama za vidole kwenye matukio leo hii mafwele ni nyundo mkononi na bunduki kufanya upelelezi na kutwa kucha kutisha raia wakubali makosa au wachinjwe tu yaishe, hamna akili tena wala maarifa yanayotumika
 
Tukiikomboa nchi tar 29 MaFUEL ,J4 na bashite watamtoa kifungoni Polepole.
 
Ndugu Humphrey Polepole akiwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi akiwapokea askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walipofika Lilongwe, nchini Malawi kutekeleza amri ya Amiri Jeshi Mkuu.

Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walipeleka msaada wa kibinadamu kwa Serikali ya Malawi – chakula na vifaa vya kujihifadhi na kujiokoa kwa wananchi wa Malawi waliokumbwa na kimbunga FREDDY.

Kimbunga FREDDY kilichosababisha mafuriko yaliyoikumba nchi ya Malawi, kilitokea 13 Machi, 2023 na kusababisha madhara mbalimbali ikiwemo majeruhi, vifo vya zaidi ya watu 400, makazi, mali, miundombinu

Msaada wa kibinadamu uliotolewa ni pamoja na fedha taslim na vifaa mbalimbali thamani ya US$1,000,000. Chakula (unga) tani 1,000. Blanketi 6,000. Mahema 50. Helicopters 2 za kijeshi. Askari 100. US$300,000

Nataka kusema kwamba, mtu ambaye ametumikia Taifa kwa kiwango hiki hastahili kutekwa na kupotezwa. Hata kama yapo makosa ambayo anadhaniwa kutenda na kuvunja sheria, akamatwe na ashtakiwe.

Mtu ambaye amewahi kuhudumu kama mwenezi wa CCM Taifa, Mbunge wa Bunge la Tanzania, Mkuu wa Wilaya, hatakiwi kutekwa na kupotezwa kwa makosa ambayo ametenda – kama yapo. Utaratibu ufuatwe, ashtakiwe.

Soma historia ya nchi hii na chama tawala (TANU-ASP/CCM), utapata majibu ya ki-muktadha ktk jambo hili.
 
Vile vile, Si vzr ukiwa chini ya kiapo cha utumishi wa umma kama hcho ukaanza kuibagaza serikali yako iliyokupa hayo mamlaka ya uwakilishi..
Huo ni uasi na ni usaliti, bila kujali alimpokea nani alistahili kupgwa risasi..
Hakuna serikali inaweza kuvumilia ujinga huo..

INATAKIWA AACHE MAIGIZO YA KUJITEKA AENDE ARIPOTI KWA MAMLAKA ILI AHOJIWE KWA UASI WAKE WA KIAPO ALIOUFANYA.
 
Huyu jamaa alikuwa ni Mkomunisti asiyependa matajiri.
 
Ndani ya CCM kuna makundi mawili ya ideology ktk mambo ya uchumi, hili kundi la kina Polepole unalo sema mara nyingi huwa lina tafsiriwa hivyo, binafsi sina hakika kama kweli wana chuki na matajiri, ila hatua zao za kiuongozi hupelekea taswira hio kujitokeza.
 
Back
Top Bottom