SoC02 Mtu Makini

Stories of Change - 2022 Competition

Makininick

New Member
Joined
Sep 2, 2022
Posts
4
Reaction score
3
Mtu huwa makini afanyapo jambo kwa juhudi na uangalifu wa hali ya juu. Mwanafunzi anayesoma kwa bidii anaonekana na umakini katika kusoma kwake, mfanyabiashara anayejituma kwenye biashara yake tunamwita mfanyabiashara "Makini".

Mtu makini huwa na malengo anayotaka kuyafikia, na hufanya juhudi kuyafikia.

Mtu makini huwa na muda maalum kufikia malengo yake, mtu makini, husikiliza wengine na kuwaelewa kabla ya yeye kujieleza. Mtu makini huwa na marafiki wa ukweli, anaoweza kuwaambia mambo yake na kupata ushauri kutoka kwao.

Mtu makini hujali hali ya roho yake, hali ya afya ya mwili wake na hupenda kuongeza elimu.

Najitahidi kua makini kwa kila ninachofanya ili kujenga jamii ya watu makini, KUA MAKINI.
 
Upvote 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…