Mtu mmoja awa albino baada ya kutumia Metakeflin

Metakeflin eeeh!?

Zamani kidogo nilifanya ujinga kwenda uzunguni huko na Malaria. Kufika huko Malaria ikaniwakia na dawa hakuna. Nikaagiza Metakeflin kutoka Tanzania DHL overnight. Zikafika nikaenda nazo kwa daktari. Weeee !!!

Niliambiwa eti zilishapigwa marufuku na zina madhara makubwa kwenye ubongo. Nilinyang'anywa dawa zangu na nikaagiziwa dawa zingine. Nilijitahidi kunywa vinywaji kwa wingi huku nikiwa monitored. Dawa imekuja kufika ikanikuta Malaria yenyewe imeshachoka. Miaka zaidi ya 10 sasa sijaugua Malaria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…