Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
- Thread starter
-
- #21
Wengi ukiwapima unakuta hakuna kitu 'special' wanachofanya; ndio maana changamoto haziishiIna maana hujaona kazi wafanyazo. Kuna wahasibu madaktari wahandisi walimu na wengineo kila mmoja na sekta yake.
Ni Kama pesa tu. Kila mtu na matumizi yake.
Ni kufanya nini, na mpaka sasa wamefanya kitu gani ambacho mtu wa darasa la nne B hawezi kufanya?
Mtu msomi ni mwanazuo aka scholar. Msomi ni Mtaalam kwenye nyanja au fani maalum.Msomi ni nani?Jibu linalokuja, ''You are incompetent you can't argue with a professor?''
Katika kusoma makala mbalimbali pamoja na kufanya tafiti binafsi, kumeonekana kuna changamoto katika kusema fulani ni msomi.
Wapo wanaoamini, katika kufikia hatua fulani ya elimu anakuwa yuko sahihi kuitwa msomi.
Wengine wanaamini msomi, ni yule anayetumia rasilimali vitu, watu, fedha na kutengeneza fursa pamoja na kutatua changamoto za jamii.
Wengine wanaamini, kuwa na utitiri wa vyeti vingi ndio njia sahihi ya wao kuitwa wasomi.
Ilibidi nichimbue zaidi vitabu na makala mbalimbali, ili kupata mitazamo tofaui tofauti kuhusu neno msomi.
Na uchambuzi wangu, umejikita kwa makundi haya katka mtazamo wa neno msomi:-
Ambao hawakwenda shule kabisa
Hili kundi wanaamini mtu msomi, ni yule aliyeajiriwa au kuongea kiingereza au mtu mwenye mali.
Ambao wanajua kusoma na kuandika
Hapa niliwatazama wale waliofanikiwa sana kuliko walioenda shule, hawa mtazamo wao wanamchukulia mtu msomi kama mtu aliyeenda shule ili kuweza kujinusuru na changamoto za maisha kwa kuajiriwa; wao wanaona wasomi kama watu wanaopindisha mambo ili waweze kujihami na ugumu wa maisha.
Ambao wana elimu ya kawaida
Hapa niliwatazama wale waliohitimu elimu ya sekondari mpaka 'degree' moja. Wao wanaamini msomi ni yule mtu anayeweza kuchambua mambo; kwa hiyo kama kati yao wanaweza kuchambua mambo, anakuwa yuko sahihi kuitwa msomi.
Ambao wana elimu ya juu
Hapa niliwatazama wenye elimu ya 'masters' na PhD; katika kundi hili wengi wao wanaamini wao ni wasomi na wako sahihi kuitwa wasomi; katika kuhoji kwa nini wanashindwa kutatua chamgamoto za kijamii ingawa wao wapo na wanajiita wasomi; wengi hutoa visingizio vingi, mara ''lack of capital, lack of skilled labour, lack of power, lack of government support n.k''
Ambao wako level ya u-professor
Hili ndio kundi la mwisho linaloamini wao ndio wasomi zaidi na hakuna mtu anayeweza kuwa-'challenge' kama hujafikia hatua yao ya kielimu.
Ni kweli ni hatua ya juu ya kielimu, lakini swali lilikuwa, ni kwa nini mpaka leo katika vyuo vyetu bado tunatumia vitabu vingi kutoka kwa wazungu iwe ni ''financial management, managemeni in general, law, operation management n.k''.
Pia, uwepo wao unawasaidiaje jamii katika kutatua changamoto zao?
Hapa nilipo sijielewi wakuu; nipeni jibu, mtu msomi ni nani?
Ni sawa na fani ya ufundiNenda pale muhimbili au hospital kubwa yoyote ukaulize wagonjwa Hao madaktari wenye Elimu za juu wanafanya kitu gani ambacho darasa la nne B hawezi kufanya.
Au siku ukiumwa au Mkeo akihitaji upasuaji ndio uulize Hilo swali.
Au muulize Maxence Mello hao Watu wa degree wanafanya nini ambacho Darasa la nne B hawawezi mpaka humu ndani tunachati
Tunazungumzia usomi sio kutatua Changamoto.Wengi ukiwapima unakuta hakuna kitu 'special' wanachofanya; ndio maana changamoto haziishi
Wengi tumeudhuria madarasani tukaondoka na magamba tu, leo hii tukiambiwa tutetee usomi wetu, tunabaki tukijing'ata ng'ata tu
Na mpaka aitwe msomi anatakiwa atimize nini au afanye kitu gani kitakachomtambulisha kimataifa?Mtu msomi ni mwanazuo aka scholar. Msomi ni Mtaalam kweneye nyanja su fani maalum.
Ukikumbuka utuletee mrejesho, wengi tunajiita wasomi wakati si wasomi.Nimesahau kidogo kuna siku Prof.Shivji alieleza tofauti ya msomi na mwanazuoni.
Ni sawa na fani ya ufundi
Kwa nini vijana wengi wako nje na taaluma zao wakisaka ajira?Sasa hapo labda ni Wewe.
Usomi unatetewa vipi Kaka,
Mpe kazi MTU inayol alichosomea, mlipe Pesa inayolingana na Elimu yake kisha uone Elimu ya mtu
Anatakiwa afanye kitu gani 'unique' tuseme huyu ni msomi; kuwa na makaratasi mengi sio usomi.Fundi WA nini?
Kila fundi analevel yake. Akifikisha kiwango cha shahada anaitwa Msomi.
Kuna Hadi shahada ya ushonaji, upishi, n.k
Hao sio wasomiTunazungumzia usomi sio kutatua Changamoto.
Hata mjinga anaweza kuwa na kitu special lakini hakimfanyi kuwa msomi.
Ili uwe msomi inabidi uende shule kwenye mfumo rasmi.
Anatakiwa afanye kitu gani 'unique' tuseme huyu ni msomi; kuwa na makaratasi mengi sio usomi.
Vyeti na Degrees vya elimu kutoka nchi mbalimbali zinatambulika kimataifa sema zinatofautiana kwa ubora. Ni kwenda shule tu mkuu.Na mpaka aitwe msomi anatakiwa atimize nini au fanye kitu gani kitakachomtambulisha kimataifa?
''Accordance with eqnx ..../ according to eqn x...'' kama kwenye maandiko ya watu, hutumiki kwenye hiyo ''phrase'', usijihangaishe kujiita wewe ni msomi.Upekee hausomewi, upekee ni natural.
Usomi sio kuwa unique.
Msomi ni kuwa na Elimu ya juu katika fani Fulani. Huo ndio usomi.
Kwa sasa Elimu ya juu ni shahada,
Alafu kuna Elimu ya juu zaidi ambazo zinahusisha mabingwa, wabobevu n.k.
Ukisimama katikati ya watu warefu, lazima ujione wewe ni mfupiHivi kumbe mimi elimu yangu ya kawaida
Na ili uwe msomi unatakiwa utumie nguvu za ziada katika kujijengaVyeti na Degrees vya elimu kutoka nchi mbalimbali zinatambulika kimataifa sema zinatofautiana kwa ubora. Ni kwenda shule tu mkuu.