Utajiri unapimwa kwa assets(mali) ulizonazo, kwa ufupi kabisa ASSETS = LIABILITIES + EQUITY....... Yaaani Mali(asset)zako ni jumla madeni yako(liability) + mtaji wako(Equity)
Mkopo ni LIABILITY lakini sio mbaya kama unavyodhani, ntaeleza hapa.
Kukopa kiTAJIRI ni pale unakopa then unaconvert part kubwa ya mkopo kuwa assets(mali) mf: biashara, mitambo, ardhi, majengo, hatimiliki etc. na sehem ndogo kuwa matumizi ya kawaida.
Kukopa kiMASKINI ni pale unapokopa then unaconvert part kubwa ya mkopo kuwa matumizi ya kawaida(expenses) mf: matanuzi na bata, kutoa misaada, safari za gharama, manunuzi ya vitu vinavyokwisha thamani haraka etc. na sehem ndogo kuwa mali.
So kujibu swali lako, mwenye deni la Trillioni 100 ni tajiri kuliko mwenye cash Billioni 100 kama alikopa kiTAJIRI kwa sababu atakuwa na mali zenye thamani kubwa kuliko mwenye cash ya Bil.100.
Ukitaka kuelewa hili, chunguza vitabu vya mahesabu vya makampuni makubwa na matajiri wote unaowajua.
Sent using
Jamii Forums mobile app