- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Nimewahi kusikia mtu akikung'ata akiwa na hasira anaweza kukuachia sumu ambayo inaweza kukuathiri, athari hutegemeana na kiwango cha hasira atakachokua nacho.
Je, kuna ukweli wowote?
Je, kuna ukweli wowote?
- Tunachokijua
- Sumu ni dutu yoyote inayoweza kuharibu kiasi kidogo shughuli za seli au inayoweza kudhuru muundo wa seli au kiumbehai.
Inaweza kunyweka, kuliwa, au kufyonzwa kupitia ngozi. Uharibifu kawaida hufanyika na mmenyuko wa kemikali. Athari ya sumu hutofautiana na kiasi ambacho kilichukuliwa mwilini. Dutu ambazo ni sumu huweza kusababisha kifo.
Kung'ata kwa binadamu hutokea wakati meno ya binadamu yanapogusana kwa mgandamizo na ngozi ya binadamu mwingine.
Je, ni kweli binadamu mwenye hasira huwa na sumu inayoweza kudhuru akimng'ata mwingine?
Kitendo cha kung'ata meno hufanywa zaidi na watoto wadogo japo mara chache watu wazima huwang'ata wengine hasa wakiwa na hasira na mara nyingi hutokea wakiwa kwenye ugomvi.
Kitendo hiki si kizuri kwani huweza kujeruhi na kusababisha mtu kupata maambukii ya magonjwa iwapo atakutana na damu ya aliyeng'ata lakini pia kinywa cha binadamu huwa na bakteria wengi ambao iwapo wataingia kwenye jeraha huweza kusababisha madhara.
Katika kufuatilia iwapo binadamu anaweza kuwa na sumu ambayo inaweza kusababisha madhara kwa binadamu kama akimnga'ata mtu akiwa na hasira, Jaiicheck ilimtafuta mtaalam wa Afya, Dkt. Bakari Nzobo Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Kinywa na Meno, Wizara ya Afya ambaye amesema Si kweli kwamba binadamu huwa na sumu iwapo akimng'ata mtu akiwa na hasira kwani binadamu hana sumu.
"Hapana, binadamu hana sumu kwenye meno au mate. Hivyo uking'atwa na binadamu mwenye hasira hauwezi kupata sumu"
"Madhara yatokanayo na kung'atwa na binadamu yapo kama vile; kukatwa ulimi, kukatwa mdomo wa chini au juu, kidonda kwenye shavu au mkono baada ya kung'atwa na meno ya mtu mwingine".
"Ikiwa umejeruhiwa kwa kung'atwa na binadamu mwenzio nenda Hospitali ili uweze kutibiwa jeraha ambalo utakuwa umelipata kutokana na kung'atwa na binadamu".
Kufuatia majibu ya Kitaalamu Jamiicheck imejiridhisha kuwa taarifa za meno ya binadamu kuwa na sumu si za kweli.