Nivea
JF-Expert Member
- May 21, 2012
- 7,460
- 4,771
[h=1]BABA NA MWANA MKOANI SINGIDA WAJERUHIWA VIBAYA NA NYEGERE.[/h]Kikoje mpwa tupiamo picha
Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 82 na mtoto wake wa kiume wakazi wa kijiji cha Nkhoiree tarafa ya Ihanja wilayani Singida, wamenusurika kufa baada ya kuvamiwa na nyegere na kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za miili yao.
Mzee huyo Ikaku Jingu na mtoto wake Julius (50),wamelazwa wodi namba tatu katika hospitali ya mkoa iliyopo mjini Singida.Nyegere ambaye anadaiwa kuwa na wivu wa mapenzi kuliko wanyama wote chini ya jua, umbo lake linafanana la paka na chakula chake kikuu ni asali.
Akizungumza na MblogI jana Alhamisi kwenye hospitalini hiyo,Mzee Ikaku amesema alikumbana na dhahama hiyo Agosti 30 mwaka huu saa sita za usiku.
Amesema akiwa amelala peke yake kwenye nyumba yake,alisikia kelele ya mnyama zikitokea kwenye zizi lake na kuamua kufungua mlango kwa lengo la kufahamu ni mnyama gani huyo.
Kwanza nilidhani kuwa kelele hizo ni za fisi, lakini nilipofungua mlango, nilimwona mnyama mdogo mwenye ukubwa unaofanana na paka akinikimbilia kwa kasi kubwaalisema.
Mzee huyo, aliongeza kuwa kwa vile alikuwa amebeba fimbo,alimpiga na nyegere huyo hadi akaamua kurudi nyuma. Lakini ghafla alimrudia tena na kuanza kumparua kwa makucha na kumuuma mikononi na miguuni.
Hata hivyo,alisema alipata nafasi akampiga tena kwa nguvu na kukimbia na ndipo alipopata nafasi ya kujikokota hadi ndani ya nyumba yake ya tembe, na kufunga mlango.
Huyu mnyama mimi binafsi amenishangaza sana jinsi alivyokuwa na hasira na nguvu nyingi kiasi hicho.Baada ya kurudi na kugundua mlango umefungwa,alipanda juu ya nyumba yangu ya tembe na kuanza kufukua udongo niliouezekea pamoja na kutoa mapawa (miti) hadi akatoboa na kutumbukia ndanialifafanua mzee Ikaku.
Akielezea zaidi mkasa huo Mzeehuyo amesema baada ya kutumbukia ndani,alipambana naye tena na alipozidiwa nguvu,alipiga yowe la kuomba msaada kwa mtoto wake Julius.
Mzee Ikaku alisema Julius alipofika,akaanza kupambana naye na kwa vile alikuwa amebeba blanketi zito,alimshauri amfunike nyegere huyo ili waweze kupata nafasi ya kutoroka.
Alisema nyegere huyo alipofanikiwa kutoka kwenye blanketi hilo,alikimbilia nyumba ya jirani lakini alishindwa kuingia ndani kwa vile imeezekwa kwa bati.
Nasikia usiku wa kuamkia septemba mosi,nyegere huyo alifika nyumbani kwangu tena na alipokosa binadamu,alivamia kichaja ninachohifadhia mahindi na kuyamwaga yote chini na kisha kuyasambaza katika eneo pana,alisema.
Mzee Ikaku anasema tukio hilo limemshangaza mno kwa vile kwa umri wake huo mkubwa, hajawahi kuona wala kusikia uvamizi mkubwa namna hiyo kufanya na nyegere.
Bila shaka nyegere huyu atakuwa na kichaa,ni vema wataalam wa wanyapori wakalifuatilia tukio hili ili kubaini iwapo mnyama huyo mdogo ana kichaa au laa,alisema mzee Ikaku.
aione Baba V na Preta hahahahahaahahah
Last edited by a moderator: