Mtu ukikutana na simba au chui ghafla porini tahadhari ni ipi?

Mtu ukikutana na simba au chui ghafla porini tahadhari ni ipi?

Hawa wanyama hawapendi ksbisa nyama ya mbuzi. Cha kufanya lia kama mbuzi, meeeee meeeeee, watakupita kama hawakuoni
 
tembea na kiberiti,,,,,pia hakikisha nguo zako zananuka petrol ili ukiiona simba au chui jipige kiberit....mwisho wa maneno....swali je ukikutana na chatu?

chatu haujamuona yeye kakuona ...duuh
 
Hivi mmeshamuelekeza namna ya kujilinda na nyegere.......au mbuni.....?....porini kubaya jamani........

wale wanyama wadogo hawana madhara unawatisha wanakimbia wenyewe
 
Nishasikiaga habari za huyu nyegere kwamba ukiwa porini ukimtaja tu huyoo..tena wakaenda mbali zaidi wakadai wanapenda zaidi "HASHUA"..kwamba wanazinyofoa.

hashua nini-tafsiri tafadhali
 
Naanza na Chui; Ni mnyama anayependa kujitenga na muda mwingi anapenda kupumzika juu ya mti au chini ya vichaka vichaka vizito vizito/ambavyo havipitishi mwanga mpaka ndani. Kutembea kwake ni pale tu anapoenda kutafuta chakura/mawindo na hapendi usumbufu. Unapomuona Chui gafla na yeye hajakuona eye to eye contact we inamisha kichwa chako au angalia sehemu nyingine huku ukiendelea na safari yako. Pale mtakapogonganisha macho chakwanza akili mwake ni kujihami maana anajua umeenda pale kumuwinda yeye na anajua asipokuwa utamuwahi yeye. Chui ana asiri ya ufuatiliaji, akikuona na kama hujamuona anaweza kukufuatilia umbal wa hata 1km bila wewe kutambua kuwa nyuma yako anakufuatilia nia ni kujua huyu mtu ana nia mbaya nami au vip, akijiridhisha kuwa hawezi kupata madhara kutoka kwako anajiachia zake huyo.
Simba; Ni mnyama anayependa kutembea kimagrupu, ukimuona simba mmoja basi jua ndani ya mita 50 kuna simba mwingine au wengine. Mara nyingi hujigawanya pale wanapofanya mawindo maana wakiwa wanawinda hawapendi kukimbia umbari mrefu so wanajigawanya ili kupunguza usumbufu wa kupata windo lao hata kama windo litakimbilia upande flan basi hukuo kunakuwa na mwingine wa kumuinterupt huyo windo. Simba ana aibu sana mbele ya binadamu na ukikutana nae usioneshe uwoga wala kutetemeka wala usigeuke na kumpa kisogo simama mwangalie eye to eye contact mwishowe huyo atapotea zake. Nadhan nimekusaidia kidogo kwa nilichojifunza juu ya hawa wanyama.

darasa huru
 
Hao viumbe ni RAHISI sana kuwashinda ukikutana nao USIOGOPE kwani they sense fear uoga wako ndio Nguvu yao na Kutokuogopa kwako ndio Weakness yao ngoja nikupe siri

Hakuna mnyama mbaya sana na hatari wa kumugopa duniani kama BINADAMU
ila hao wengine sijui taka taka gani hamna kitu

 
Last edited by a moderator:
Hahaha, daah huyo mlinzi mwingine alikua bandidu maana hakuona eneo jingine la kusimika mshale zaidi ya mku.nd


Naye alikuwa ni mtaalam wa kuua wanyama pori. Huyu jamaa (mbondei wa Turiani) alikuwa anasema kwao kuua simba ama chui si hoja kwani hata watoto wanaua chui na hawaogopi kutembea maporini usiku.
 
Ukiweza kuelewana na kukaa karibu na mbwa mwitu utakuwa umeondokana na madhara ya simba. Chui siyo msumbufu lakini jifunze kulenga na uwe na shabaha kwelikweli. Chukua rungu hata ile ya kimasai-"Ruguma" unapokabiliana na chui we wahi kumtandika kichwani ni dhaifu sana mnyama yule. Hukuulizia Nyegere kama alivyogusia Preta, aisee mnyama yule anajua wewe ndo unampuguzia asali kule porini. Kwa kweli utamtabua...tembea na debe la asali pengine atakusamehe.
 
Last edited by a moderator:
chui hana madhara sana kwa binaadamu ukilinganisha na simba. ni watu wengi sana huku kwetu wamekutana na chui billa madhara yoyote
 
Back
Top Bottom