Mtu ukikutana na simba au chui ghafla porini tahadhari ni ipi?

Mtu ukikutana na simba au chui ghafla porini tahadhari ni ipi?

Kwa simba ujasiri wako tu ndio silaa yako. Wewe jifanye chizi tu, akija mputa mputa tulia anza kumchezea chezea sharubu. Anamtindo baada ya mda mfupi hujitenga na wewe kando. Hapo angalia mti mrefu wenye tawi zuri panda. Tabu yake akikumaindi atatoka chini ya huo mti. Anamkwara wa kufa mtu, anaweza akawa ananguruma hapo, lazima uharo ukutoke. Usipokuwa jasiri utadondoka juu ya huwo mti. Omba watu wa jirani ulipo wasikie kilio chako la sivyo kwa heri.

Kwa upande wa chui, wewe piga magoti tu. Akija mputamputa mkumbatie na umbusu, ataanza kucheza na wewe. Tatizo la chui akianza kucheza na wewe utakiwi kuchoka, ukichoka tu niagieni niagieni unakwenda kwa baba yao, utarudi milele. Unatakiwa usichoke huku ukiomba kwa mola wako upate msaada wa kumfanya Chui ale kona.

oooh my god!
 
Kuishi porini inakupasa kuwa jasiri sana usiogope First time naingia Ruaha NP nilikua n'a woga kama wako it takes few hours Nawe unakua jasili kama simba. Sheria kuu ni hii... USIWASUMBUE NAO HAWATAKUSUMBUA. Usipige kelele ukiwa porini hata kama huoni chochote, hakikisha kila mlango wako wa fahamu unafanya kazi vizuri, tembea kwa utaratibu, wenyeji wako watakubrief Ratiba za wanyama wap sa ngapi mnyama gani n'a mambo mengine kibao. Usiogope coz utakua n'a hofu sio nzuri porini. Wanyama wachumi wazuri hawapotezi nguvu kupambana n'a kitu kisichowadhuru. Jiamini usimpe simba mgongo mkazie macho tuu. Chui mstaarabu sana n'a sio rahisi kumuona anajitenga sana n'a wakati wote anaamini haonwi..jitahidi asijue kuwa umemuona akijua majanga sana..anapenda maeneo ya machaka matulivu n'a msitu msitu maeneo kama hayo kuwa makini sana. Nyati hatari wanaonaonekana kirahisi n'a wakorofi sana wengine ila hawashambulii kirahisi usiwachokoze. Tembo hanaga shida sana coz maeneo mengi wenyeji wanajua tabia zao utajuzwa. Njoka wabaya sana coz wana sumu hakikisha unavaa boots n'a unaangalia unapokanyaga...usishike miti hovyo baadhi yao wanakaa juu ya miti. Jikite kwenye kazi yako usizulule porini hatari. Mengine utajuzwa ukifika

nashukuru mkuu kwa mtazamo mzuri
 
Ni vema umeuliza ili ujuwe ukweli. Kumbuka, adui mkubwa wa mnyama ni binadamu na adui mkubwa wa binadamu ni binadamu mwenziwe. Usiwe mwoga wa mnyama yeyote, kama kweli unataka kwenda kuishi porini kuwa na silaha za kukulinda ila si viwembe wala sindano ya kushonea nguo. Kuna uwezekano mkubwa sana chui akikuona atakufuata bila wewe kujuwa na huenda asikudhuru because they are curious by nature, ila simba akikuona na akijuwa umemuona atakukimbia na asirudi tena ile sehemu iwapo atajuwa binadamu anaishi hapo bcs by nature simba wako shy na hawapendi mtafaruku na binadamu. Nakuhakikishia this, nyoka usimuhofie hata awe nyoka wa aina gani labda awe wa kutumwa tu ndiyo anaweza kukudhuru. Usisikilize habari za vijiweni kuhusu nyoka....nina elimu kubwa sana juu ya nyoka kitaaluma na wala si kijiweni. Nyoka ni mwoga sana kwa binadamu, na kama ukienda sehemu yeyote ambayo kuna nyoka usijisumbue kumtafuta huyo nyoka. Kama unajuwa huyo nyoka yuko hapo, wewe ongea kama vile unapiga kelele kwa dakika kama mbili hivi then nyamaza halafu angalia ile sehemu. Lazima utaona huyo nyoka au hao nyoka wanaondoka kwa kukimbia kwani wanajuwa lile eneo basi limeshaingiwa na binadamu. Nyoka atakuuma tu pale anapokuwa cornered na hana jinsi ila hata iweje hakuna nyoka wa aina yeyote duniani anayewinda binadamu porini, huo ni uwongo. Nyoka before anakuuma wewe, will always try to run away from you first. Zamani wakati niko mdogo nilikiaga uwongo mwingi sana juu ya koboko na ukali wake na jinsi anavyowinda watu huko porini, nikawa mwoga sana. Then baada ya kwenda shule nikakutana na jamaa (mwanafunzi wa herpatology) aliyekuwa anasomea ophiology (study of snakes), nikamsumulia nyoka waliopo hapa Tanzania pamoja na zile hadithi za koboko nilizokuwa nasikia wakati niko mdogo. Jamaa akanicheka sana na akaniambia hakuna kitu kama hiko hapa duniani. Sikuamini. Nikaja naye hapa Tanzania likizo kwa mwezi na nusu tukaenda mpaka maporini na jamaa alikuwa anakamata nyoka balaa, tena si kwa mitego ila kwa mikono. Tukawa Moyowosi kule Kigoma ambako kuna koboko balaa, jamaa alituacha hoi, yaani alipanda juu ya mti kumkamata koboko ambaye alikuwa anakimbia, hii ilikuwa mwaka 2001. Baada ya kupata somo la koboko na nyoka wengine kwa kweli sihofii nyoka yeyote hapa duniani nina elimu ya kutosha.

nimekupata
mkuu habari hii ni muhimu kwangu
 
Nakuhakikishia ukikutana nae ghafla face to face yule mnyama atakuua tu hata akikupa nafasi ya kujitetea, mana hata ukijitetea yule mnyama hajui kiswahili. Labda utembee na bastola yenye risasi za kutosha muda wote.

Ahahahahahaaa mbavu zangu. Anajua lugha gani mkuu?
 
wanyama wote ni wakawaida sana ndio maana wanafugwa, mbaya ni binadamu ka alqued anakuua alau hakutumii, kama chakula. chui ni muoga kweli usikubali kumpa kisogo, akiruka kukudaka wahi mikono ya mbele, simba huyo muwahi ulimi kwani huwa hawezi kurudi nyuma anakua pale pale
 
tembea na kiberiti,,,,,pia hakikisha nguo zako zananuka petrol ili ukiiona simba au chui jipige kiberit....mwisho wa maneno....swali je ukikutana na chatu?
 
Hivi mmeshamuelekeza namna ya kujilinda na nyegere.......au mbuni.....?....porini kubaya jamani........
 
sala ni muhimu ila ishara za huyo mnyama sitaki anidhuru
Sala ni muhimu kwa kila kitu. Ishara gani tena mkuu unazungumzia!? Au Simba na Chui wakiwa wanakuja kukudhuru huwa wanaKUDIP (beep)!!??
Kama umeenda kuishi PORINI utakuwa umewafuata nyumbani kwao mkuu kwa hiyo huwezi kuwaepuka ni kuwa makini tu. Ni sawasawa na kwenda Bar ukaagiza mzinga wa Konyagi peke yako halafu useme Sitaki kulewa.
 
we chukua nguo kisha washa moto nasikia huwa wanatoka nduk cha muhimu ni kutembea na all sources of fire
 
Hivi mmeshamuelekeza namna ya kujilinda na nyegere.......au mbuni.....?....porini kubaya jamani........

Nishasikiaga habari za huyu nyegere kwamba ukiwa porini ukimtaja tu huyoo..tena wakaenda mbali zaidi wakadai wanapenda zaidi "HASHUA"..kwamba wanazinyofoa.
 
Hakikisha unamuakia...shkamooo uncle simba/chui...!baada ya hapo atakuona una nidhamu na kukuacha!!!haya kimbia sasa wahi huko porini tushakupa maujanja....

Jaman nimecheka kama mwehu hapa!! Mpaka machozi yametiririkaaaaaa......
 
Nishasikiaga habari za huyu nyegere kwamba ukiwa porini ukimtaja tu huyoo..tena wakaenda mbali zaidi wakadai wanapenda zaidi "HASHUA"..kwamba wanazinyofoa.

huyu mnyama nasikia ni rafiki sana na jinsia ya kiume...........bora ukutane na pride nzima ya simba kuliko nyegere mmoja.........kidudu kina kisasi kama binadamu vile...........
 
Hao viumbe ni RAHISI sana kuwashinda ukikutana nao USIOGOPE kwani they sense fear uoga wako ndio Nguvu yao na Kutokuogopa kwako ndio Weakness yao ngoja nikupe siri
Hakuna mnyama mbaya sana na hatari wa kumugopa duniani kama BINADAMU
ila hao wengine sijui taka taka gani hamna kitu

Unavyoongea utafikiri ushawahi kukutana na nyati vile!hebu kamsalimie pale mdonya -ruaha halafu jifanye uogopi,nenda selous kamtusi mama kiboko uone,pita serengeti kamshike ---- baba simba then uje tuambia kuwa ulisalimika kwa kuwa ulikuwa huwaogopi!hiyo siri yako baki nayo mwenyewe !hayawani ni hatari na wakalie mbali!
 
Ukikutana na Simba au Chui ghafla porini, Kama ni Mkristo usali sala ya Baba Yetu...Kama ni Muislam piga kelele ya Allah hu Akbar na Kama ni mpagani chagua nyimbo yoyote ya Diamond au Joto hasira muimbie Simba au Chui labda atakuonea huruma. Kila la kheri huko porini.

teh teh,we jamaa
 
Naanza na Chui; Ni mnyama anayependa kujitenga na muda mwingi anapenda kupumzika juu ya mti au chini ya vichaka vichaka vizito vizito/ambavyo havipitishi mwanga mpaka ndani. Kutembea kwake ni pale tu anapoenda kutafuta chakura/mawindo na hapendi usumbufu. Unapomuona Chui gafla na yeye hajakuona eye to eye contact we inamisha kichwa chako au angalia sehemu nyingine huku ukiendelea na safari yako. Pale mtakapogonganisha macho chakwanza akili mwake ni kujihami maana anajua umeenda pale kumuwinda yeye na anajua asipokuwa utamuwahi yeye. Chui ana asiri ya ufuatiliaji, akikuona na kama hujamuona anaweza kukufuatilia umbal wa hata 1km bila wewe kutambua kuwa nyuma yako anakufuatilia nia ni kujua huyu mtu ana nia mbaya nami au vip, akijiridhisha kuwa hawezi kupata madhara kutoka kwako anajiachia zake huyo.
Simba; Ni mnyama anayependa kutembea kimagrupu, ukimuona simba mmoja basi jua ndani ya mita 50 kuna simba mwingine au wengine. Mara nyingi hujigawanya pale wanapofanya mawindo maana wakiwa wanawinda hawapendi kukimbia umbari mrefu so wanajigawanya ili kupunguza usumbufu wa kupata windo lao hata kama windo litakimbilia upande flan basi hukuo kunakuwa na mwingine wa kumuinterupt huyo windo. Simba ana aibu sana mbele ya binadamu na ukikutana nae usioneshe uwoga wala kutetemeka wala usigeuke na kumpa kisogo simama mwangalie eye to eye contact mwishowe huyo atapotea zake. Nadhan nimekusaidia kidogo kwa nilichojifunza juu ya hawa wanyama.
 
Ndugu yangu nimepata darasa kubwa sana kwako, naweza kuamini usemacho maana kuna movie moja ya kisouth Africa inaitwa Mr. Bones, pale kuna sehem Vince Lee alikuwa anamuokoa mpenzi wake mbele ya simba, alichofanya jamaa ni kumkazia mimacho simba na kumtisha as if anaunguruma huku akijifanya anataka kumparamia, simba akawa kama anaona aibu akatimua mbio kwenda mapangoni. Hilo la chui nlikuwa sijua ndo nimepata darasa kwako kiongozi. JF unapata burudani (kwa comments ridiculous za baadhi ya watu), unacheka, na pia unapata darasa la kutosha, kila nikipitia nyuzi za humu natoka na kitu kichwani ambacho nilikuwa sijui. Viva JF.
 
Naanza na Chui; Ni mnyama anayependa kujitenga na muda mwingi anapenda kupumzika juu ya mti au chini ya vichaka vichaka vizito vizito/ambavyo havipitishi mwanga mpaka ndani. Kutembea kwake ni pale tu anapoenda kutafuta chakura/mawindo na hapendi usumbufu. Unapomuona Chui gafla na yeye hajakuona eye to eye contact we inamisha kichwa chako au angalia sehemu nyingine huku ukiendelea na safari yako. Pale mtakapogonganisha macho chakwanza akili mwake ni kujihami maana anajua umeenda pale kumuwinda yeye na anajua asipokuwa utamuwahi yeye. Chui ana asiri ya ufuatiliaji, akikuona na kama hujamuona anaweza kukufuatilia umbal wa hata 1km bila wewe kutambua kuwa nyuma yako anakufuatilia nia ni kujua huyu mtu ana nia mbaya nami au vip, akijiridhisha kuwa hawezi kupata madhara kutoka kwako anajiachia zake huyo.
Simba; Ni mnyama anayependa kutembea kimagrupu, ukimuona simba mmoja basi jua ndani ya mita 50 kuna simba mwingine au wengine. Mara nyingi hujigawanya pale wanapofanya mawindo maana wakiwa wanawinda hawapendi kukimbia umbari mrefu so wanajigawanya ili kupunguza usumbufu wa kupata windo lao hata kama windo litakimbilia upande flan basi hukuo kunakuwa na mwingine wa kumuinterupt huyo windo. Simba ana aibu sana mbele ya binadamu na ukikutana nae usioneshe uwoga wala kutetemeka wala usigeuke na kumpa kisogo simama mwangalie eye to eye contact mwishowe huyo atapotea zake. Nadhan nimekusaidia kidogo kwa nilichojifunza juu ya hawa wanyama.
Mkuu,
Hapo kwenye Red umenipoteza kidogo. Hao Simba wenye aibu wako pori gani mkuu? Au ni Simba wa kinyaturu?
Kuna binadamu gani,let alone MTANZANIA wa kuweza kumwangalia uso kwa uso au macho kwa macho!!??? Maana haya Mapaka ya huku uswahilini tu yanatutoa Jasho kuyaangalia machoni sembuse ukikutana na Simba mkuu.
Haya mambo ya Indiana Jones tuyaache kwenye sinema tu ndugu zangu. Asilimia 80 ukikutana na Simba ana kwa ana itakuwa ndio Ze Endi.
 
Back
Top Bottom