Ni vema umeuliza ili ujuwe ukweli. Kumbuka, adui mkubwa wa mnyama ni binadamu na adui mkubwa wa binadamu ni binadamu mwenziwe. Usiwe mwoga wa mnyama yeyote, kama kweli unataka kwenda kuishi porini kuwa na silaha za kukulinda ila si viwembe wala sindano ya kushonea nguo. Kuna uwezekano mkubwa sana chui akikuona atakufuata bila wewe kujuwa na huenda asikudhuru because they are curious by nature, ila simba akikuona na akijuwa umemuona atakukimbia na asirudi tena ile sehemu iwapo atajuwa binadamu anaishi hapo bcs by nature simba wako shy na hawapendi mtafaruku na binadamu. Nakuhakikishia this, nyoka usimuhofie hata awe nyoka wa aina gani labda awe wa kutumwa tu ndiyo anaweza kukudhuru. Usisikilize habari za vijiweni kuhusu nyoka....nina elimu kubwa sana juu ya nyoka kitaaluma na wala si kijiweni. Nyoka ni mwoga sana kwa binadamu, na kama ukienda sehemu yeyote ambayo kuna nyoka usijisumbue kumtafuta huyo nyoka. Kama unajuwa huyo nyoka yuko hapo, wewe ongea kama vile unapiga kelele kwa dakika kama mbili hivi then nyamaza halafu angalia ile sehemu. Lazima utaona huyo nyoka au hao nyoka wanaondoka kwa kukimbia kwani wanajuwa lile eneo basi limeshaingiwa na binadamu. Nyoka atakuuma tu pale anapokuwa cornered na hana jinsi ila hata iweje hakuna nyoka wa aina yeyote duniani anayewinda binadamu porini, huo ni uwongo. Nyoka before anakuuma wewe, will always try to run away from you first. Zamani wakati niko mdogo nilikiaga uwongo mwingi sana juu ya koboko na ukali wake na jinsi anavyowinda watu huko porini, nikawa mwoga sana. Then baada ya kwenda shule nikakutana na jamaa (mwanafunzi wa herpatology) aliyekuwa anasomea ophiology (study of snakes), nikamsumulia nyoka waliopo hapa Tanzania pamoja na zile hadithi za koboko nilizokuwa nasikia wakati niko mdogo. Jamaa akanicheka sana na akaniambia hakuna kitu kama hiko hapa duniani. Sikuamini. Nikaja naye hapa Tanzania likizo kwa mwezi na nusu tukaenda mpaka maporini na jamaa alikuwa anakamata nyoka balaa, tena si kwa mitego ila kwa mikono. Tukawa Moyowosi kule Kigoma ambako kuna koboko balaa, jamaa alituacha hoi, yaani alipanda juu ya mti kumkamata koboko ambaye alikuwa anakimbia, hii ilikuwa mwaka 2001. Baada ya kupata somo la koboko na nyoka wengine kwa kweli sihofii nyoka yeyote hapa duniani nina elimu ya kutosha.