Mtu ukikutana na simba au chui ghafla porini tahadhari ni ipi?

Kikoje mpwa tupiamo picha
[h=1]BABA NA MWANA MKOANI SINGIDA WAJERUHIWA VIBAYA NA NYEGERE.[/h]
Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 82 na mtoto wake wa kiume wakazi wa kijiji cha Nkhoiree tarafa ya Ihanja wilayani Singida, wamenusurika kufa baada ya kuvamiwa na nyegere na kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za miili yao.​
Mzee huyo Ikaku Jingu na mtoto wake Julius (50),wamelazwa wodi namba tatu katika hospitali ya mkoa iliyopo mjini Singida.
Nyegere ambaye anadaiwa kuwa na ‘wivu wa mapenzi’ kuliko wanyama wote chini ya jua, umbo lake linafanana la paka na chakula chake kikuu ni asali.
Akizungumza na MblogI jana Alhamisi kwenye hospitalini hiyo,Mzee Ikaku amesema alikumbana na dhahama hiyo Agosti 30 mwaka huu saa sita za usiku.
Amesema akiwa amelala peke yake kwenye nyumba yake,alisikia kelele ya mnyama zikitokea kwenye zizi lake na kuamua kufungua mlango kwa lengo la kufahamu ni mnyama gani huyo.
“Kwanza nilidhani kuwa kelele hizo ni za fisi, lakini nilipofungua mlango, nilimwona mnyama mdogo mwenye ukubwa unaofanana na paka akinikimbilia kwa kasi kubwa”alisema.
Mzee huyo, aliongeza kuwa kwa vile alikuwa amebeba fimbo,alimpiga na nyegere huyo hadi akaamua kurudi nyuma. Lakini ghafla alimrudia tena na kuanza kumparua kwa makucha na kumuuma mikononi na miguuni.
Hata hivyo,alisema alipata nafasi akampiga tena kwa nguvu na kukimbia na ndipo alipopata nafasi ya kujikokota hadi ndani ya nyumba yake ya tembe, na kufunga mlango.
“Huyu mnyama mimi binafsi amenishangaza sana jinsi alivyokuwa na hasira na nguvu nyingi kiasi hicho.Baada ya kurudi na kugundua mlango umefungwa,alipanda juu ya nyumba yangu ya tembe na kuanza kufukua udongo niliouezekea pamoja na kutoa mapawa (miti) hadi akatoboa na kutumbukia ndani”alifafanua mzee Ikaku.
Akielezea zaidi mkasa huo Mzeehuyo amesema baada ya kutumbukia ndani,alipambana naye tena na alipozidiwa nguvu,alipiga yowe la kuomba msaada kwa mtoto wake Julius.
Mzee Ikaku alisema Julius alipofika,akaanza kupambana naye na kwa vile alikuwa amebeba blanketi zito,alimshauri amfunike nyegere huyo ili waweze kupata nafasi ya kutoroka.
Alisema nyegere huyo alipofanikiwa kutoka kwenye blanketi hilo,alikimbilia nyumba ya jirani lakini alishindwa kuingia ndani kwa vile imeezekwa kwa bati.
“Nasikia usiku wa kuamkia septemba mosi,nyegere huyo alifika nyumbani kwangu tena na alipokosa binadamu,alivamia kichaja ninachohifadhia mahindi na kuyamwaga yote chini na kisha kuyasambaza katika eneo pana”,alisema.
Mzee Ikaku anasema tukio hilo limemshangaza mno kwa vile kwa umri wake huo mkubwa, hajawahi kuona wala kusikia uvamizi mkubwa namna hiyo kufanya na nyegere.
“Bila shaka nyegere huyu atakuwa na kichaa,ni vema wataalam wa wanyapori wakalifuatilia tukio hili ili kubaini iwapo mnyama huyo mdogo ana kichaa au laa”,alisema mzee Ikaku.

aione Baba V na Preta hahahahahaahahah
 
Last edited by a moderator:
Mwanadamu ndio kiube Mwenye mamlaka ya kutawala viumbe vyote Dunia na sifa kubwa ya Mwanadamu tumepewa Akili ya kutambua Kila kitu! Ingawa na hivi viumbe vina Akili kwa baadhi ya mambo lakini mwanadamu ndio kiboko Yao
Tumia Akili yako yote na mbinu zako bila kusahau kua wewe ndo Mwenye mamlaka ya kutawala Kila kitu!
 
baba yangu mdogo alikuwa anatabia ya ulevi uliopindukia ,sasa siku moja usiku wa manane alikutana na chui,hakuangaika nae ,yule chui alimfuata 3kms mpaka anaingia ndani kwake nae akageuza akaondoka .

Many thanks to Viloba that he had that night.
 

Hako kamdudu kasenge kweli... Yaani kanaondoka kanakwenda kujifikiria afu kanarudi kufanya "revenji" :frusty::frusty:
 

Kwa madhara, chui anaweza kuua watu hata mia kwa dakika1! Kivipi? Ni kwamba chui ni mnyama aliejaaliwa kutembea ardhini na juu kama vile kima, nyani, sokwe na jamii hizo. Sasa, kama watu muko hamsini au hata mia, chui aweza kutembea vichwani huku kucha zake akiwa amezifungua na hivyo kuacha ubongo ukiwa wazi kabisa, na ni jambo la muda mfupi tu, watu wote ni maiti. Tifauti na simba ambae ataua mmoja hadi mwingine kwa kutumia maguvu na ubabe. Chui ni hatari zaidi akiamua kudhuru kuliko simba! Simba anakula watu, chui hali, ila ni muuaji mzuri
 
Atamjualia wapi koboko,mtu kazaliwa na kukulia k.koo??


Hiki kizazi cha dotcom kujifanya hawajuwi vitu vya kiafrika, kwa kweli wanakera. Sitashangaa mtoto wa dotcom akauliza what is a chicken kana kwamba huko mitaani hawaoni wanazagaa. Hiki kizazi kweli ni alosto.
 



Mku tafadhali usilete myth au legends zisizo na akili. No way na haijawahi kutokea chui kuua hata watu wawili kwa dakika moja au tano labda hao watu wawe watoto wa miezi kadhaa wasio na uwezo wa kujikinga na chui. Watu tunaua chui for as a sport (ila kimagendo). Kule Turiani tuna shamba la ukoo na mifugo, chui kibao na mara kwa mara tunawaona nje ya uzio ila wakithubutu tu kuua mbuzi basi roho yao ni yetu. Ni vizuri hatujuani kimacho na sura, kule tuna ngozi na vichwa vya chui karibia 6, na tunapowawinda tunakuwa si zaidi ya 4. Siku moja chui alimrukia mlinzi wetu shingoni baada ya kukoswa na mshale. Jamaa akapiga kelele ndipo mlinzi mwenzake alipoenda na kusimika mshale mkunduni mwa chui na kukata kata utumbo mpaka chui kufa, mbona hakumtoa ubongo yule mlinzi? Haya mambo ya vijiweni kwa kweli yanapotosha sana watu na kuwa wawoga bila sababu. Chui hana madhara kihivyo, tena anaweza kukuona na wala asikudhuru labda uwe umekaribia watoto wake ndipo atakudhuru ili kuwalinda watoto wake.
 
Wakuu huenda nikaenda kuisha mazingira ya porini na nimekua nikisikia kuhusu wanyama wa kali ni hatari je hatua zipi nichukue kukabiliana na majanga tofouti tofauti nikiwa huko?

we ukiwaona uzibe mdomo wako na uzibe pua ili wasisikie harufu ya binadamu, hakyanani lazima akupite hivihivi
 
Labda, kutegemea na maeneo. Ila kwa kule kusini , chui ni wachache, ila ni tishio hasa.
 

duh! Mwanangu hicho cha arusha nn?
 
Labda, kutegemea na maeneo. Ila kwa kule kusini , chui ni wachache, ila ni tishio hasa.

Mkuu umetembea Tanzania lakini? Kusini mwa Tanzania ni hatari ndugu yangu mbona wanyama hatari ni wengi mno? Umesahau kule kuna Selous na mapori ya hajabu yaliyojawa wanyama wa kutisha?
 
Mkuu umetembea Tanzania lakini? Kusini mwa Tanzania ni hatari ndugu yangu mbona wanyama hatari ni wengi mno? Umesahau kule kuna Selous na mapori ya hajabu yaliyojawa wanyama wa kutisha?

Nafaham, kwa kuwa huko ndiko chimbuko langu, na chui anaheshimika na kuogopwa sana na wenyeji, ndipo nikasema kutegemea na maeneo au species za hao chui, ila kule kusini Mtwara na Lindi chui ni wakali sana. Nadharia ya chui kudhuru watu100 kwa muda mfupi kuliko simba ni ya kweli kabisa, ila matukio hayo ni nadra. Chui huwa hapendi kuonekana!
 
Labda, kutegemea na maeneo. Ila kwa kule kusini , chui ni wachache, ila ni tishio hasa.


Mkuu kusini kuna chui balaaa. Hivi hujuwi kusini kuna mapori na Selous iko kule? Unasema kusini ya wapi?
 
Ukikutana na hao wanyama we jin.ye.e tu!


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hahahahaha!
 

Hahaha, daah huyo mlinzi mwingine alikua bandidu maana hakuona eneo jingine la kusimika mshale zaidi ya mku.nd
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…