Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni mtihani sana.Mtoa mada analalamika watu na heshima zao wanatoka na wake za watu bila kujua hao wake za watu ukiwakuta barabarani huwezi tofautisha na malaya wa kimboka kwa alivyovaa sasa kwa hali hiyo wataachaje kutongozwa
Mke kweli anatakiwa awe tofauti na anaetafuta bwana au malaya kuanzia kujiheshimu na mavazi hapo hata lugha ya kuingilia huna ila hawa vichenchede wa asaivi hata sio wake za watu ila ni vimada vilivyowekwa ndani na wanaume kadhaa
Mtu unamuheshimu Kabisaaa lakini anatembea na mke wa mtu na anajua ni mke wa mtu.
Hivi unajisikiaje kuwa sehemu ya migogoro katika ndoa ya mwanaume mwenzako?,sawa inawezekana umejua kuwa ndoa ya huyo mwanamke ina tafrani, je migogoro ya ndoa ya mwingine ni ticket ya wewe kumtaka na kutengeneza mgogoro ktk ndoa yako kama unayo?.
Ok utakuta mume wa mtu lakini ana date na mke wa mtu tena kwa mahaba mazito, hivi unachukuliaje kuwa sehemu ya kuvunja moyo wa mkeo pindi atakapo tambua?.
unajisikiaje kuwa mzurumati wa amani na furaha ya ndoa yako mwenyewe?,
Ok sawa, tufanye unakosa Haki zako za msingi kutoka kwa mkeo, hivyo huna budi kutoka nje, sasa kwanini ukatembee na mke wa mtu kwani hakuna walio mali ya umma ?
Nikweli sisi wanaume tuna udhaifu lakini inawezekana kuuzuia ili tusiumize mioyo ya hawa wanawake ambao tayari ni wake zetu, tuwe walinzi wa ndoa za wengine kama vile tulindavyo zetu.
Kuna mwanamke anamume tena anajiheshimu ,lakini anamchepuko ambaye ni mume wa mtu, na ukimwambia wewe ni mke wa mtu anakwambia kwani mke wa mtu ni kitu gani?
Sawa inawezekana ndoa yako ina migogoro hivyo unaitafuta furaha nje, sasa upi ni ulazima wakuitafuta furaha kupitia mume wa mwanamke mwenzako?, au furaha nikuona ndoa yake inakuwa kama yako?
Huoni kwamba unahujumu amani na furaha ya ndoa ya mwanamke mwenzako?, sisi wanaume hatuna uwezo wakusambaza furaha na kupenda mwanamke zaidi ya mmoja ,ni mbwembwe tu, hivyo ukiona anakuoenda ujue amesha hamisha upendo kutoka familia na mke wake, hivyo kaacha maumivu Yale ambayo huyahitaji na kamuachia mwanamke mwenzake.
Unajisikiaje kuwa sababu ya kilio na maumivu kwa mwanamke mwenako??
Kama unaona ndoa yako haikupi thamani basi achana nayo ili utengeneze thamani yako nje ya ndoa, na kama ndoa inakupa thamani basi ilinde hiyo thamani.
TUJISAHIHISHE.