Mtu wa kunisaidia kuipata simu yangu

Islam005

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2008
Posts
3,354
Reaction score
3,623
Wadau habari zenu, simu yangu iliibiwa juzi kati mtu alichomoa dirishani. Sasa nimeicheck kwa kutumia google inaonekana mara ya mwisho ilisomeka maeneo fulani(napajua) pia nimeitumia Samsung Find ambayo inaweza kupata location ya device hata ikiwa offline na inaonekana ipo maeneo fulani ambayo sio mbali sana na ninapoishi.

Nahitaji mtu(ikiwa ni polisi itakuwa bora zaidi) ili kufuatilia zaidi especially hili eneo la mwisho.

Loss report na imei number vyote ninavyo ila pia chochote hakitakosekana kama simu ikipatikana, nisaidieni kabla haijauzwa mbali zaidi.
Location ni Dar Kigamboni
 
Pole mkuu, kwanza huwezi pata huyo mtu atakayeitrack bila kumlipa kwanza ata awe polisi lazima utamlipa kwanza, kuna mambo atayafanya ya gharama kdg mfano nakufunulia code kidogo(atakua ana move hapa na pale kufatilia issue yako, hii ni nauli na vocha kutrack hivi na vile, sasa apo lazima umpe kianzio, cha kukushauri kama una imani nenda polisi especially kama upo dar nenda kituo kikubwa kuna maaskari wema tu, nje ya hapo tutakudhulumu huku mtandaoni na simu utachelewa kuipata au usiipate kabisa, wahi polisi mpe ata 30k ya nauli afatilie jambo lako
 
Fika kituo Cha Police kilicho karibu Nawe.

Siyo lazima uzingatie; ila ukifika Police chonga nao vizuri wape hela ya maji wakishamdaka huyo simbilisi arudishe gharama zako then waambie police na wao wajipatie chochote kitu kabla ya kumwachia
 
Acha upumbavu,, nenda polisi idara ya Cyber security ndio kazi yao hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…