Mtu wako wa karibu anakwambia nini katika hatua kama hii?

et "mpo" ... nyie wanawake wa jamiiforum ambao kila muda tunawasoma humu na mentality zenu za ovyoo sijui mambo yakienda mrama ndani ya familia mume ndio chanzo!! kuwa na aibu hata kama tunatumia fake ids
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kumbe zinawaingia eeeh!! Na bado.
 
Ni kweli kabisa "ukiona mambo yanakaenda mrama ujue kichwa cha familia kimeshindwa kusimamia nafasi yake".
 





Ulimwengu tunaoishi unaongozwa na kanuni. Moja ya kanuni kubwa ni kanuni ya KUPANDA na KUVUNA. Utavuna ulichopanda; na utavuna mema kama ulipanda mema; na ukipanda mabaya basi jiandae kuvuna mabaya. Na katika kupanda mema au mabaya; sio lazima uje uvune kwa mtu yule yule ulikopanda; wakati mwingine utavuna kwa third party; Au usivune wewe wakavuna kizazi chako.

Unfortunately; Wengi wetu hatujali nini tunapanda; bali tunatarajia sana mavuno mema tena hata ambako hatukupanda. Unaishi na mwenzi wako; humjali, unamnyanyasa, kumdhalilisha, unamnenea maneno mabaya etc; then siku ya uhitaji wako unatarajia uvune huruma na loyalty yake; je kwake ulipanda huruma na loyalty?

Huku kwetu most of times mke ukikamatwa unachepuka ni hakuna maelezo talaka 3; la kumnyanyasa me ni kwa ke wachache na wanalimudu hilo effectively. Ila mume kuchepuka eti ni nature; so mke utavumilia tu; ukinyanyaswa; ukipigwa, ukiletewa watoto vumilia tu.You have a face to save to the society; maana utaambiwa mwanamke mjinga huvunja ndoa yake blah blah. Bado wengi wetu ni tegemezi; unawaza ntaanzaje maisha on my own; what about my kids etc. So pamoja na manyanyaso yote bado utaendelea kudumu ndoani. Unfortunately katika manyanyaso haya; wanawake wengi huwa wanaishia kubeba uchungu moyoni. Uchungu ambao unaweza ukawa unamtafuna yeye mwenyewe; mwingine uchungu anamalizia kwa watoto; yani ni mkali kwa watoto na watadundwa hao bila hata kosa la msingi. Wachache huwa wanaomba rehema juu ya waume zao; hadi kufikia hatua ya kuwasamehe; ilhali bado wanawaumiza

Wale wenye uchungu; siku yako ya tabu ndo siku ya yeye kutoa uchungu wake; aisee utasuffer (sio kama unakukomoa; ile mimba ya uchungu ndo inatoka; so vumilia tu). Unfortunately tunaishiaga kulaani tu hawa wanaotoa uchungu wao; bila kujiuliza ndani yao kulipandwa nini. Do you expect anything good to come out of a bitter person? Hata neno la Mungu linasema "Moyo uliochangamka ni dawa nzuri"; so moyo wa mkeo uliojikunja juu yako huo, utakuwa ni ugonjwa kwako. Msamaha ni kwa wachache walio na neema; hawa watakusaidia despite maumivu yote uliyowapa. Uchungu zaidi unakuja pale ambapo mnarudigi kwa wake zenu mkishakuwa total liabilities kwao; either umefulia kabisa au ndo unaumwaaa. Mke lazima uchungu uzidi; lazima akumbuke ulivyomtosa wakati things were ok for you; sasa hivi umebaki kushney karonga ndo unamuona mwema? Umegundua wema wake, ukajuta ndo ukamrudia au umerudi kwa sababu huna option? Thats hurts so so much. Afu msamaha haulazimishwi; it is earned slowly. Make some efforts hadi mkeo ajue huyu kweli amejuta.

Kukosea sawa; ila rejeeni kwa wake zenu wakati hali bado ni shwari. Na wao waexperience "katika raha"; sio wao kila siku ni katika shida tu; raha na wengine eeeeh. "UNAPANDA NINI"?
 
Pasua kichwa nilikumiss[emoji3531]
Hawa viumbe wana kumbukumbu fupi sana linapokuja jambo linalohusu wanawake. Ila inapokuja kwao sasa wanavyojitiisha huruma na kukumbuka vifungu vya Biblia utashangaa!!

Watulie tuu wavune wanayoyapanda muda wa mavuno ukifika.
Ndio maana huwa nawaambia ukiona familia inayumba jua kichwa cha familia hakijielewi.
 
Hapana. Nilikuwa nakusaidia tu kuwa kwenda PM kwa RR kusingekusaidia chochote. Hawezi kukupa taarifa yangu yoyote; angekurudisha kwangu obviously
That was different, I wasn't going to inquire anything about you. I wanted to ask him something and for that he was the best person for me to ask.

Utashtuka nkikwambia i don't need to ask anything about because i already know you.
 
One of the best coment....Barikiwa.

Atoto hongera kwa malezi mazuri.
 
I want to call all those who said JF imejaa wanawake wajinga ili waje waone hii. Kwenye ile list yangu ya wanawake kumi makini humu jukwaani amini kwamba na wewe umo.

Congrats boss
 
Tukikosa jicho la rohoni ndio mnatakiwa mzidi kutuombea mkeshe kabisa tufunguliwe maana maombi yenu yananguvu.
Hoyeeeeeee!!
Hakika tunastahili sifa, ni wanaume wanaojielewa pekee wanaoweza kutuelewa. Inahitaji jicho la rohoni and bad enough wengi hawana.
Haleluyaaaa!
 
Kwa hapa Tz ' Wanawake wenye Tabia njema Hiyo. ..tayari walisha kufa Katika Vita ya Kagera
Muone vileeeee mfyuuuuuuuuuu..... Tatizo ni nyinyi wenyewe mtu unajitoa kwa moyo wote..... Unakubaliana na hali zote ukiwa unajua huyu ni mwanaume /mume wangu... Mnakuja kulipa malipo ya hovyohovyo
 
Hahaha haaaa haa. .akikuchoka zaidi anakuambia yule John ndiye mwanaume mwenye akili sasa ''
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa upande wangu zaidi ya kuambiwa "siwezi kuoa mwanamke maskini" sijawahi ambiwa neno zuri la faraja


Ila mungu yupo wallah naomba mungu amuweke yule kijana ashuhudie maajabu yake uuuwiiii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…