Ulimwengu tunaoishi unaongozwa na kanuni. Moja ya kanuni kubwa ni kanuni ya KUPANDA na KUVUNA. Utavuna ulichopanda; na utavuna mema kama ulipanda mema; na ukipanda mabaya basi jiandae kuvuna mabaya. Na katika kupanda mema au mabaya; sio lazima uje uvune kwa mtu yule yule ulikopanda; wakati mwingine utavuna kwa third party; Au usivune wewe wakavuna kizazi chako.
Unfortunately; Wengi wetu hatujali nini tunapanda; bali tunatarajia sana mavuno mema tena hata ambako hatukupanda. Unaishi na mwenzi wako; humjali, unamnyanyasa, kumdhalilisha, unamnenea maneno mabaya etc; then siku ya uhitaji wako unatarajia uvune huruma na loyalty yake; je kwake ulipanda huruma na loyalty?
Huku kwetu most of times mke ukikamatwa unachepuka ni hakuna maelezo talaka 3; la kumnyanyasa me ni kwa ke wachache na wanalimudu hilo effectively. Ila mume kuchepuka eti ni nature; so mke utavumilia tu; ukinyanyaswa; ukipigwa, ukiletewa watoto vumilia tu.You have a face to save to the society; maana utaambiwa mwanamke mjinga huvunja ndoa yake blah blah. Bado wengi wetu ni tegemezi; unawaza ntaanzaje maisha on my own; what about my kids etc. So pamoja na manyanyaso yote bado utaendelea kudumu ndoani. Unfortunately katika manyanyaso haya; wanawake wengi huwa wanaishia kubeba uchungu moyoni. Uchungu ambao unaweza ukawa unamtafuna yeye mwenyewe; mwingine uchungu anamalizia kwa watoto; yani ni mkali kwa watoto na watadundwa hao bila hata kosa la msingi. Wachache huwa wanaomba rehema juu ya waume zao; hadi kufikia hatua ya kuwasamehe; ilhali bado wanawaumiza
Wale wenye uchungu; siku yako ya tabu ndo siku ya yeye kutoa uchungu wake; aisee utasuffer (sio kama unakukomoa; ile mimba ya uchungu ndo inatoka; so vumilia tu). Unfortunately tunaishiaga kulaani tu hawa wanaotoa uchungu wao; bila kujiuliza ndani yao kulipandwa nini. Do you expect anything good to come out of a bitter person? Hata neno la Mungu linasema "Moyo uliochangamka ni dawa nzuri"; so moyo wa mkeo uliojikunja juu yako huo, utakuwa ni ugonjwa kwako. Msamaha ni kwa wachache walio na neema; hawa watakusaidia despite maumivu yote uliyowapa. Uchungu zaidi unakuja pale ambapo mnarudigi kwa wake zenu mkishakuwa total liabilities kwao; either umefulia kabisa au ndo unaumwaaa. Mke lazima uchungu uzidi; lazima akumbuke ulivyomtosa wakati things were ok for you; sasa hivi umebaki kushney karonga ndo unamuona mwema? Umegundua wema wake, ukajuta ndo ukamrudia au umerudi kwa sababu huna option? Thats hurts so so much. Afu msamaha haulazimishwi; it is earned slowly. Make some efforts hadi mkeo ajue huyu kweli amejuta.
Kukosea sawa; ila rejeeni kwa wake zenu wakati hali bado ni shwari. Na wao waexperience "katika raha"; sio wao kila siku ni katika shida tu; raha na wengine eeeeh. "UNAPANDA NINI"?