Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 1,237
- 1,744
Mathayo 26:14-15 TKU
[14] Ndipo Yuda Iskariote, mmoja wa wanafunzi kumi na wawili wa Yesu alikwenda kuzungumza na wakuu wa makuhani. [15] Akasema, “Nikimkabidhi Yesu kwenu, mtanilipa nini?” Makuhani walimpa sarafu thelathini za fedha.
Yuda alikuwa mtu wa karibu sana na Yesu, haikutegemewa kama angeweza kuwaendea makuhani na kupata wazo la kumsaliti Yesu kwa ahadi ya kupewa kiasi chochote cha fedha alichokitaka.
Alichotaka Yuda ni kipi atapata akiwaonyesha Yesu, inaonyesha wazi Makuhani walikuwa na utata ni yupi halisi kati ya wanafunzi wake 12.
Yuda alipopata majibu ya kile alichokuwa anakitafuta na kukabidhiwa kiasi cha fedha, kuanzia hapo akawa anasuka mipango ya kukamatwa kwa Yesu.
Mathayo 26:16 TKU
[16] Kuanzia siku hiyo, Yuda alianza kutafuta muda mzuri wa kumsaliti Yesu.
Wapo watu wanasubiri wapate kitu wanachokitata kisha wakusaliti, wanaonyesha ukaribu na upendo wa bandia kwako kwa sababu hawajapata kile wanachokitaka.
Siku wakijiwa na maadui zako wanaweza kutoa taarifa zako zote zinazohitajika kwao, utajikuta unakamatwa huko huko ulipokuwa unafikiri upo salama.
Mathayo 26:48-49 TKU
[48] Yuda aliyekuwa amkabidhi Yesu kwao, alipanga kufanya kitu cha kuwajulisha yupi kati ya wafuasi alikuwa Yesu. Alisema, “Mtu nitakayembusu ndiye mtakayemkamata.” [49] Hivyo Yuda alikwenda kwa Yesu na kumwambia, “Salamu, Mwalimu!” Kisha akambusu.
Tunapata somo kubwa sana hapa, unayefikiri ndiye rafiki wako wa kweli, unayefikiri mnaheshimiana sana na kutoka naye mbali, na unayefikiri hawezi kukusaliti kutokana na mnavyoheshimiana, anaweza akawa mtu wa kwanza kukuuza kwa maadui zako kwa bei anayoitaka.
Hupaswi kuamini rafiki yako kiasi cha kujiaminisha kila kitu kwake na kumpa siri zako zote, anaweza kutumika vibaya na adui zako.
Adui zako hawaogopi na hawaoni hasara kumtimizia haja zake rafiki yako wa karibu aliyebeba siri zako nyingi, tamaa ikimwingia ujue umepotezwa.
Akina Yuda tunao wengi sana katika jamii zetu, tunao makanisani, kwenye maofisi, na kwenye familia zetu, wapo kila kona, tena ni watu usio na mashaka nao kabisa.
Binadamu anaweza kuingiwa na tamaa mbaya muda wowote, hupaswi kuweka imani yako yote kwake, zaidi weka imani kwa Mungu wako.
Nasema hivyo kwa sababu wapo watu ni wazuri sana kwako wakiwa hawajaingiwa tamaa mbaya, siku wakiacha kuwa na hofu ya Mungu, na kuruhusu tamaa zao za mwili ziwaendeshe, ujue umeumia/umekwisha.
Sikuambii haya uache kufanya kazi na watu, vyema kujua lolote linaweza kutokea kwa mtu wa karibu, hii ikupe tahadhari na kuwekeza imani yako kwa Mungu zaidi. Yeye hawezi kukusaliti na ulinzi wake ni bora zaidi.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana